1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yajitoa kwenye mkataba wa CFE

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cb1z
** FILE** Russian President Vladimir Putin, right, and First Deputy Prime Minister Dmitry Medvedev, background second, left, visit the village of Tavrovo in the western Belgorod region, on Thursday, Sept. 13, 2007. Dmitiry Medvedev, whose candidacy for Russian leader got the endorsement of President Vladimir Putin, on Tuesday, Dec. 11, 2007, suggested that Putin become prime minister after the March 2 election. (AP Photo/RIA Novosti, Vlaladimir Rodionov, Presidential Press Service)
Rais wa Urusi,Vladimir PutinPicha: AP

Urusi kuanzia usiku wa manane wa Jumatano, imeachana rasmi na makubaliano ya kudhibiti vikosi vya kawaida barani Ulaya:kwa ufupi Mkataba wa CFE.

Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Maghribi-NATO inasikitishwa na uamuzi wa Urusi kujitenga na mkataba wa kudhibiti vikosi barani Ulaya.Wakati huo huo Shirikisho la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya OSCE limesema,mkataba huo ni nguzo ya usalama wa eneo la Bahari ya Atlantik na Bara Ulaya.Urusi imeombwa kufikiria upya uamuzi wake wa kujitoa kwenye mkataba unaozuia usambazaji wa majeshi ya kawaida barani Ulaya.

Lakini vilio hivyo ni kama unafiki kwa sababu nchi za Ulaya na Marekani zilikuwa na nafasi ya kutosha kuchukua hatua za kuzuia mkasa huo.Kwani Urusi,mara kwa mara ilitoa mito ya kufanya majadiliano,hata kama hatua hiyo ilikuwa kwa manufaa yake yenyewe kama propaganda ya uchaguzi. Vile vile kulikuwepo muda wa kutosha,kabla ya kufikia tarehe ya mwisho iliyopangwa na Urusi kujitoa kwenye mkataba huo.

Kwa haki,nchini Urusi wanauliza kwanini,nchi nyingi za NATO hadi hivi sasa hazikuidhinisha rasmi Mkataba wa CFE uliorekebishwa kuambatana na hali mpya ya kisiasa kufuatia kusambaratika kwa Soviet Union ya zamani.Ikiwa kweli mkataba huo ni muhimu,mbona haukuidhinishwa na nchi hizo hata baada ya kuitia vishindo Urusi kwa mfano kuondosha vikosi vyake kutoka Georgia.

Je matamshi ya wanasiasa wa Kimarekani kuhusu mkataba huo yapimwe vipi,viongozi hao wanaposema kuwa Marekani ina haki ya kuweka makombora na vyombo vya kijeshi ko kote itakapo?Urusi ingetamka hayo,basi sauti zingepazwa duniani.

Nchini Urusi,sura inayoibuka huonyesha kuwa mipaka ya Urusi inazidi kukaribiwa na NATO na vile vile silaha zinazidi kurundikwa katika nchi zisizo katika Makubaliano ya CFE.

Na mpango wa Marekani kutaka kuweka mitambo ya kujikinga dhidi ya makombora nchini Poland na Jamhuri ya Czech ulivuka mpaka wa ustahmilivu. Serikali ya Urusi inataka majadiliano kwa sababu inahisi usalama wake unahatarishwa.

Wanasiasa na hata viongozi wa kijeshi wa ngazi ya juu wanasisitiza kuwa hawana mpango wa kuimarisha silaha au vikosi moja kwa moja.Hata ikiwa mipango ya aina hiyo ingeungwa mkono na wazalendo.Zaidi ni matumaini kuwa kwa kuzidisha vishindo,nchi za magharibi zitarejea katika meza ya majadiliano.
Urusi ingependelea kuwa na mkataba mpya.Wito ni: Haki sawa kwa wote.Hilo ni dai linaloeleweka, ikiwa mkataba huo wapaswa kubakia nguzo ya usalama kama ilivyoelezwa na OSCE.Mpira upo nchi za NATO na sasa zinapaswa kuthibitisha jinsi mkataba huo ulivyo muhimu kwa nchi hizo.