1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama kwanza; Obama ateua mawaziri wake wa mambo ya kigeni na ulinzi.

Sekione Kitojo2 Desemba 2008

Rais mteule wa Marekani Barack Obama afanya uteuzi wa nafasi muhimu za kiusalama.

https://p.dw.com/p/G7Ry
Rais mteule Barack Obama kushoto amesimama na waziri mpya wa mambo ya kigeni pamoja na James Jones mshauri wa masuala ya kiusalama.Picha: AP

Rais mteule wa Marekani amefanya uteuzi wake katika nafasi muhimu za kiusalama. Katika uteuzi wake amemteua pia mpinzani wake mkubwa katika kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha urais na chama cha Democratic , Hillary Clinton, kuwa waziri mpya wa mambo ya kigeni na waziri wa sasa wa ulinzi Robert Gates ataendelea kushikilia wadhifa huo.

Tangazo hilo lililokuwa linasubiriwa kwa hamu ni ushahidi wa juhudi za rais huyo mteule , za kujaribu kujenga sera zake za masuala ya kiusalama.



Usalama kwanza, unasema msemo mmoja maarufu wa Kijerumani. Na hii pia ndivyo inavyoonyesha rais mteule wa Marekani Barack Obama anavyoiangalia hali. Uteuzi wake wa watu katika nyadhifa za waziri wa mambo ya kigeni na waziri wa ulinzi pamoja na washauri wa masuala ya usalama , unaonyesha uwezo, maarifa pamoja na hisia zinazoelemea katika sera za kiusalama. Sera ambazo zinalenga katika kusafisha sera za utawala wa rais anayeondoka madarakani George W. Bush, lakini pia bila ya kuvunja umuhimu wa usalama wa taifa.


Obama asingeweza kumpata mtu imara zaidi ya Hillary Clinton katika wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni . Seneta huyo wa jimbo la New York na ambaye ni mke wa rais wa zamani wa Marekani ana uzoefu mkubwa wa masuala ya kimataifa na kwa upande wa masuala ya ulinzi uwezo wa seneta huyu umejengeka katika miaka iliyopita. Mzozo wa Iraq, mvutano wa kinuklia na Iran ama kitisho cha ugaidi wa kimataifa, changamoto hizi zitakuwa mada muhimu katika miaka ijayo kwa Bibi Clinton.

Katika wadhifa huo muhimu lakini anapaswa kuchukua hatua kwa mtazamo wa Obama , kuwa Marekani itakuwa mshirika tena na sio kama taifa kubwa lenye uwezo wa kijeshi.

Uteuzi wake unamaliza uhasama uliokuwapo katika uteuzi wa chama chao katika kiti cha urais, ambapo hali hiyo itaweza kufanikisha urais wa rais mteule.

Kitu kinachosisimua ni kwamba Hillary Clinton alikuwa anaunga mkono vita vya Iraq, kama pia waziri wa sasa wa ulinzi Robert Gates. Gates ambaye anaheshimika katika pande zote za kisiasa , alichukua wadhifa huo kutoka kwa waziri wa zamani wa ulinzi Donald Rumsfeld miaka miwili iliyopita. Tangu wakati huo ameweza kulishughulikia suala la Iraq kwa kupitishwa mkakati wa uimarishaji. Gates ni kiongozi ambaye anasisitiza mpango wenye utaratibu mzuri wa kujiondoa kutoka Iraq.

Na pia Obama inaonyesha anamawazo kama hayo. Na mengine yote anaweza kuyajenga kirahisi katika sera zake za ulinzi, na haraka kuitoa Iraq katika kitisho kingine cha kuvamiwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida.

kamanda mkuu wa zamani wa NATO James Jones bila shaka ni mtu anayefahamika. Ni mmoja wa wale ambao wameukosoa vikali utawala wa Marekani chini ya rais Bush katika vita vya Afghanistan. Kama mshauri wa taifa wa masuala ya kiusalama anao uzoefu mkubwa wa masuala ya kijeshi, ambapo anafahamu kuwa mzozo huo hauwezi kutatuliwa kwa njia ya silaha.

►◄