1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushirikiano wa dhati kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

Rais Obama aahidi ushirikiano wa dhati pamoja na Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/GfLP

Washington:


Rais Barack Obama wa Marekani ameahidi uungaji mkono wa dhati kwa Umoja wa Mataifa.Akizungumza kwa simu pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon,rais Obama ameahidi kuunga mkono kikamilifu juhudi za Umoja wa mataifa katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa,umaskini na ugaidi.Kwa mujibu wa duru kutoka ikulu ya White House,rais Obama na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon wamezungumzia pia namna ya kufanikisha shughuli za jumuia hiyo ya kimataifa. Kwa mujibu wa taarifa ya shirika rasmi la habari la China,Xinhua,serikali ya mjini Beijing inapendelea kuimarishwa uhusiano pamoja na Marekani.Uhusiano kati ya nchi hizi mbili unabidi ufuate lengo la mkakati na matarajio ya muda mrefu" amesema hayo waziri wa mambo ya nchi za nje wa China,Yang Jiechi katika sherehe za kuadhimisha miaka 30 tangu uhusiano ulipoanzishwa rasmi kati ya China na Marekani.