1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uswisi yaidhinisha kusafirisha vifaru 25 Ujerumani

22 Novemba 2023

Uswisi leo imeidhinisha kurudishwa kwa vifaru 25 Ujerumani baada ya Berlin kutoa hakikisho kwamba, haitovunja sheria za Uswisi za kutoegemea upande wowote kijeshi, kwa kuvipeleka vifaru hivyo Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ZKSY
Vifaru vikiwa katika msafara wa pamojal
Vifaru vikiwa katika msafara wa pamojaPicha: JALAA MAREY/AFP/Getty Images

Serikali ya Uswisi imetoa idhini kurudishwa kwa vifaru hivyo chapa Leopard 2 A4 kwa mtengenezaji wake halisi, kampuni ya Rheinmetall Landsysteme nchini Ujerumani.

Uswisi kwa sasa inavifaru 134 kama hivyo ambavyo vimefanywa kuwa vya kisasa na ina vifaru vingine 96 kama hivyo ambavyo haivitumii.

Soma pia:Ujerumani na Italia kufanya mkutano wa kilele Berlin

Serikali ya Uswisi imesema vifaru hivyo si vya Ukraine na hatua ya Ujerumani kuthibitisha kwamba vitasalia ndani ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO ni muhimu mno.

Msimamo wa Uswisi wa kutoegemea upande wowote kijeshi, umejadiliwa pakubwa tangu Urusi ianye uvamizi wake nchini Ukraine.