1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti wa chuo kikuu Oxford waitoa kitanzini Facebook

10 Agosti 2023

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na Chuo cha Oxford unapingana na uchambuzi wa awali na mitazamo iliyoenea baada ya kubaini hakuna ushahidi kuwa ukuaji wa matumizi ya mtandao wa Facebook umesababisha madhara kisaikolojia

https://p.dw.com/p/4V0n2
Kivuli cha mtu akiitazama nembo ya Facebook.
Kivuli cha mtu akiitazama nembo ya FacebookPicha: Rafapress/Zoonar/IMAGO

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Mtandao ya Chuo Kikuu cha Oxford, umechambua data kutoka kwa karibu watu milioni 1 katika nchi 72 kwa kipindi cha miaka 12. Uchunguzi huo umepata kile walichokiita  mahusiano mazuri  kati ya kutumia jukwaa la mitandao ya kijamii na kile walichokiita viashiria vya ustawi.

Watafiti walichanganya data ziliyokusanywa na kampuni ya utafiti ya Marekani ya Gallup kuhusu ustawi na takwimu za wanachama wa kimataifa wa Facebook, ili kutathmini ushirikiano baina ya tovuti zinavyohusiana kwenye viashiria vitatu:­-  kuridhika kimaisha, na uzoefu mbaya na mzuri wa kisaikolojia.

Soma Zaidi:Threads ya Instagram: Meta yapania kuipiku Twitter

Timu ya Oxford imesema Facebook iilitoa data yao, ambayo watafiti wake walikuwa wameichunguza kwa usahihi, japo haikuwa imefadhiliwa au kushawishi muundo wa utafiti huo ama kujua matokeo ya awali. Tafiti ambayo karatasi zake zilipata uhakiki wa masula ya rika na jarida la Royal Society Open Science.

Mwasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg.
Mwasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg.Picha: Nick Wass/AP Photo/picture alliance

Profesa wa masuala ya tabia ya binadamu na teknolojia wa Chuo Kikuu cha Oxford, Andrew Przybylski amesema walichunguza data bora zaidi inayopatikana na wakagundua hawakuunga mkono wazo la kwamba uanachama na Facebook unasababisha madhara.

Andrew aliongeza kusema ''kwa uchambuzi walioufanya umeonyesha kuwa Facebook ina uwezekano wa kuleta uhusiano mzuri na ustawi mzuri. Lakini akaweka angalizo kuwa hii si kuthibitisha kwamba Facebook ni nzuri kwa ajili ya ustawi wa watumiaji".

Watafiti kwenye mradi huo, ambao ulianza kabla ya janga la UVIKO-19, walifanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili kupata data muhimu kutoka kwa Facebook, ambayo kwa sasa inaripoti karibu watumiaji bilioni tatu ulimwenguni.

Hata hivyo, timu ya utafiti kutoka 2008 hadi 2019 ilijikita zaidi katika kuangalia namna itakavyopenya njanja za kimataifa, ikijumuisha majibu kuhusu hali ya ustawi kama sehemu ya Utafiti wa Kura ya Gallup kutoka kipindi hicho watu wakiwa 946,798.

Soma zaidi:Zuckerberg akanusha Facebook kudhuru watoto makusudi

Kwa upande wake mshiriki utafiti na mwandishi mwenza wa utafiti Matti Vuorre amesema mbinu hiyo haikuwa nzuri sana, linapokuja suala la kuchambua mitandao ya kijamii na matokeo, ingesaidia kwa kuwa na mjadala unaozunguka mitandao ya kijamii ili kuwa na mustakabali wa utafiti wenye nguvu zaidi.

Mvujishaji wa taarifa kuhusu Facebook Frances Haugen mjini Brussels.
Mhandisi wa zamani wa Facebook Frances Haugen mjini Brussels.Picha: Geert Vanden Wijngaert/AP/dpa/picture alliance

Amesema wanatofautiana na tathmini za awali, ikiwa ni pamoja na changanuzi mbili tofauti za kitaaluma mwaka jana ambazo ziligundua Facebook ilikuwa na athari mbaya kwa afya ya akili ya wanafunzi wa chuo cha Marekani, pamoja na kesi za madai nchini Marekani.

Mhandisi wa zamani wa Facebook Frances Haugen mwaka 2021, alivujisha zaidi ya nakala 20,000 za nyaraka za ndani zilizoeleza kuwa kampuni hiyo imeweka faida mbele zaidi ya usalama, na hivyo kuisababishia Marekani kuweka msukumo mpya kwa ajili ya kudhibiti.

Takribani shule 200 katika majimbo kadhaa nchini Marekani zimefungua kesi ya pamoja dhidi ya kampuni kubwa za teknolojia kwa madai ya kusababisha madhara ya kiakili, msongo wa mawazo na wasiwasi miongoni mwa wanafunzi. 

Kampuni mama ya Facebook na Instagram, Meta imekanusha madai hayo, huku mwanzilishi wake Mark Zuckerberg akidai juhudi hizo zilizoratibiwa za kutumia nyaraka zilizovuja zinalenga kuchora taswira ya uwongo.