1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uvunjaji sheria kiholela Libya kisiki kwa upatikanaji amani

John Juma
29 Machi 2022

Wachunguzi wa UN wamesema ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Libya, ikiwemo uhalifu dhidi ya ubinadamu na uvunjaji sheria kiholela unazuia mchakato wa mpito wa nchi hiyo kuelekea demokrasia na amani.

https://p.dw.com/p/49Bz7
Libyen Protest NGO
Picha: Hazem Turkia/AA/picture alliance

Kwenye ripoti yake mpya iliyotolewa Jumatatu, ujumbe huru wa uchunguzi nchini Libya umetahadharisha kuwa visa vingi vya ukiukwaji haki za binadamu, vinatishia uhuru wa uchaguzi na juhudi za kusaka demokrasia.

Mohamed Auajjar, mwenyekiti wa ujumbe huo amewaambia waandishi wa habari kwamba hakutakuwa na amani bila ya kukomeshwa kwa kadhia hizo na demokrasia haitatimia bila ya kukomesha uvunjaji sheria kiholela.

UN:Libya huenda ikawa na serikali mbili

Ujumbe huo wa watu watatu umetaja vitisho na usumbufu dhidi ya wanaharakati, mashambulizi dhidi ya mawakili na majaji pamoja na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya makundi yaliyoko katika hatari mathalan, wahamiaji, wanawake na wafungwa.

Visa vya ukiukwaji haki vimeshamiri tangu Oktoba 2021

Katika ripoti yao ya kwanza iliyotolewa mwezi Oktoba, wataalamu hao walisema visa vya mauaji,mateso, ubakaji, watu kufungwa na wengine kupotezwa kutoka magereza ya Libya, vinaweza kuchukuliwa kama uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Auajjar amesema ”tangu wakati huo wamepata ushahidi zaidi kwamba ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya wafungwa katika magereza ya Libya umeenea, ni tatizo la kimfumo au yote mawili.

Umoja wa Mataifa wajitolea kupatanisha Libya

Ripoti ya pili ya ujumbe huo imerekodi matukio yaliyotokea tangu mwezi Novemba, yakienda sambamba na mkwamo wa kisiasa kuelekea na hata baada ya tarehe ya uchaguzi ulioahirishwa.

Libya ilipaswa kufanya uchaguzi wake Disemba iliyopita kama sehemu ya mchakato unaoongozwa na Umoja wa Mataifa kumaliza mzozo ambao umedumu tangu mwaka 2011, wakati rais wa zamani wa nchi hiyo Moammar Gadafi alipouawa baada ya maandamano makubwa.

Waziri mkuu wa mpito Libya aonya uwezekano wa kuzuka vita

Ripoti yakosa kujiingiza kwenye mkwamo wa kisiasa Libya

Miongoni mwa masuala yaliyozusha mvutano Libya ni utata kuhusu wale wanaotaka kuwania urais.
Miongoni mwa masuala yaliyozusha mvutano Libya ni utata kuhusu wale wanaotaka kuwania urais.Picha: Khaled Al-Zaidy/Handout/Reuters

Auajjar amesema ujumbe huo ulioundwa na shirika la Haki za Binadam,u la Umoja wa Mataifa mnamo Juni 2020, hautazungumzia hali ya kisiasa nchini humo.

Hata hivyo ujumbe huo ulijikita zaidi kwenye visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ambavyo vimekuwa visiki dhidi ya juhudi za mpito wa nchi hiyo kisiasa kuwezesha upatikanaji wa amani, demokrasia na utawala wa kisheria.

Wataalamu hao wamesema wamepokea ripoti za kusikitisha za mashambulizi dhidi ya wanaharakati na mashirika yao nchini Libya.

Uchaguzi wa urais Libya wakumbwa na wasiwasi

Waliangazia pia mashambulizi dhidi ya wanawake wanasiasa ikiwemo kutoweshwa kwa mbunge Seham Sergiwa mnamo mwaka 2019 na vilevile mauaji ya kikatili dhidi ya wakili maarufu Hanan Al.-Barassi mnamo mwaka 2020, kuchochewa na uvunjaji sheria kiholela.

(AFPE)