1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATIKAN: Rais Bush amekutana na Papa Benedikt XVI

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtH
Rais George W.Bush wa Marekani amemuhakikishia Papa Benedikt XVI kuwa ataendelea kupiga vita UKIMWI barani Afrika.Amesema,atalishinikiza bunge la Marekani kuongeza mchango wake kupiga vita UKIMWI hadi Dola bilioni 30 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Rais Bush na mkewe hii leo kwa mara ya kwanza walionana na kiongozi wa Kanisa Katoliki katika mkutano wa faragha.Kwa mujibu wa duru za Vatikan,vita vya Irak na hali ya Wakristo nchini humo ni miongoni mwa mada zilizozungumzwa.