1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vimini marufuku kwa wafanyakazi wa umma Uganda

5 Julai 2017

Serikali imekataza magauni na sketi fupi ambazo huonesha magoti na sehemu za mapaja kwa upande wa wanawake, blauzi na mashati yanayodhihirisha vifua vya wanawake na wanaume, na kwa jumla nguo za kubana mwili.

https://p.dw.com/p/2fySl
Wanawake wenye vimini
Wanawake wenye viminiPicha: Paballo Thekiso/AFP/Getty Images

J3 05.07.2017 Uganda: Dresscode - MP3-Stereo

Hereni na bangili kubwa nazo zimepigwa marufuku kwa watumishi wakiwa kazini. Watumishi wa umma aidha waliagizwa kutovalia ndala ila tu ikiwa wanafuata ushauri wa daktari. Watu mbalimbali nchini Uganda wamepokea  agizo la mavazi ya heshima kwa watumishi wa serikali kwa maoni tofauti tofauti. Mjadala ambao umeibuka ni kama mavazi yana mahusiano yoyote na utendaji kazi wa mtu kazini na kama agizo hilo linalenga kuwanyima wanawake haki zao kujirembesha vile wapendavyo.