1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi mbali mbali washutumu hatua ya Musharraf.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79y

Wakati huo huo viongozi wa kimataifa wametoa wito kwa jenerali Musharraf , kurejesha utawala wa sheria na kuirejesha Pakistan katika demokrasia. Marekani , ambayo inamuona Musharraf kuwa mshirika wake muhimu katika mapambano yake dhidi ya ugaidi, imesema kuwa inafadhaishwa sana hatua hiyo. Maafisa wa Uingereza wameeita hatua hiyo ya hali ya hatari kuwa ni hatua ya kurudisha nyuma demokrasia nchini Pakistan. Mataifa makubwa mawili katika eneo la Asia , hata hivyo yamechukua tahadhari katika matamshi yao. China imesema kuwa ina imani kuwa Pakistan inaweza kutatua matatizo yake, wakati hasimu mkubwa wa muda mrefu India imeamua kupunguza hali ya wasi wasi baina ya mataifa hayo kwa kutoa taarifa inayosema kuwa India inasikitishwa na hali ngumu iliyomo Pakistan.