1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia wakutana

Sekione Kitojo
22 Juni 2019

Viongozi wa  mataifa  ya  kusini  mashariki  mwa  Asia wamekusanyika  mjini  Bangkok Jumamosi(22.06.2019)wakidhamiria kupatikana  kwa  mkataba  mpana  wa  kibiashara  duniani.

https://p.dw.com/p/3KtqA
Thailand Bangkok | ASEAN Gipfel der Außenminister
Picha: picture-alliance/Zuma Press/C. Subprasom

Wakati  vita  vya  kibiashara  kati ya  Marekani  na  China vikigubika muonekano wa  uchumi wa  mataifa hayo  unaoongozwa  na biashara ya mauzo ya nje.

Mizozo katika eneo tete la  bahari ya  kusini  mwa  China, uteswaji wa Waislamu wa  Rohingya  na  Myanmar na  uchafuzi  wa  taka za plastiki  katika  bahari  pia ni  masuala  yanayopangwa  kujadiliwa katika  mkutano  huo  wa  siku  mbili  wa  Umoja  wa  mataifa  ya kusini mashariki  mwa  Asia, ASEAN, chini  ya  uenyekiti  wa Thailand.

Thailand Bangkok | ASEAN Gipfeltreffen - Joko Widodo
Viongozi wa mataifa ya Umoja wa ASEAN wakiwa katika kikao mjini BangkokPicha: Biro Pers, dan Media Sekretariat Presiden

Lakini  biashara  itachukua  nafasi  ya  kati  katika  mkutano  huo wa viongozi  wa  ASEAN ambao wana  nia  ya  kuharakisha  kutiwa saini kwa  makubaliano ya  kibiashara  yaliyotayarishwa  na  China yanayowafikia  karibu nusu  ya wakaazi  wote  wa  dunia.

Makubaliano  hayo  yanayofahamika  kama  Ushirikiano mpana wa kiuchumi wa kimkoa RCEP , unajumuisha  mataifa  yote 10  ya Umoja  wa  ASEAN, pamoja  na  India, Japan, Korea  kusini , Australia  na  New Zealand.

Yanaonekana  kuwa  ni  utaratibu wa  China  kuandika  sheria  ya biashara  kwa  mataifa  ya  Asia  na  Pacifiki, kufuatia  Marekani kujitoa  kutoka  katika  eneo  hilo.

Kuwekeana  ushuru kwa kulipiza

Muda  mfupi  baada  ya  kuchaguliwa   rais  Donald Trump  aliiondoa Marekani  kutoka  ushirikiano  huo  wa  eneo  la  bahari  ya  Pacifiki , TPP, ambao  ungekuwa  ni makubaliano  makubwa  kabisa  ya biashara  duniani, akiushutumu  kuwa  unauwa  ajira  nchini Marekani.

Thailand Bangkok | ASEAN Gipfeltreffen - Joko Widodo mit Aung San Suu Kyi
Rais wa Malaysia Joko Widodo akiwa pamoja na kiongozi wa Myanmar Aung San Suu KyiPicha: Biro Pers, dan Media Sekretariat Presiden

Wakati hatua  za  kulipizana  kwa  kuwekeana  ushuru  wa  juu  kati ya  mataifa  hayo  mawili  yenye  uchumi  mkubwa  duniani zimeshuhudia  baadhi  ya  makampuni  yakiikimbia  China  na kukimbilia  katika  maeneo  mengine  ya  salama katika  mataifa  ya ASEAN, wataalamu  wa  uchumi  wanasema  picha  pana  zaidi  kwa ajili  ya  ukuaji  wa  uchumi  wa  dunia inatia  shaka.

Katika  muktadha  huo, RCEP ni muhimu  kwa  kuongeza  kiwango cha  biashara," msemaji wa  serikali  ya  Thailand Wrrachon Sukhondhapatipak  aliwaambia  waandishi  habari.

"Ni bora  zaidi iwapo makubaliano  ya  RCEP yataanza  kazi haraka," Martin M. Andanar , waziri  wa  mawasiliano  wa  Ufilipino amewaambia  waandishi  habari.

"Biashara  huru  ni  kitu  bila  shaka  tunachokihitaji  katika  kanda hii," amesema , na  kuongeza  kuwa  mzozo  wa  kibiashara  kati  ya China  na  Marekani  umesababisha , "duniani  nzima  kupata  homa".

Thailand Bangkok | ASEAN Gipfeltreffen - Joko Widodo
Rais Joko Widodo (kushoto) katika mkutano wa ASEAN mjini Bangkok , ThailandPicha: Biro Pers, dan Media Sekretariat Presiden

Hatua za  maendeleo zimesita sita  katika  miezi  ya  hivi  karibuni wakati  India  ikiweka munda kutokana  na  hofu  ya  bidhaa za bei ya  chini  za  China  kuingia  na  kufurika  katika  soko  hilo  kubwa  la nchi  hiyo.

Australia  na  New Zealand  pia zimeonesha  wasi  wasi  kuhusiana na  ukosefu wa  usaalma  wa  kazi  na  mazingira.