1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Pakistan na Afghanistan wakutana.

27 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgZf

Islamabad. Rais wa Pakistan Pervez Musharraf na mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai , wamekubaliana kuongeza ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Taliban na al-Qaeda katika mpaka baina ya mataifa hayo.

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Pakistan , Islamabad, Musharraf amesema kuwa imani kali na ugaidi vinatishia kuharibu nchi zote mbili.

Na mahitaji ya ushirikiano katika nyanja ya taarifa za kijasusi ni kubwa ili kupambana na hali hii ya imani kali na ugaidi, hali ambayo inaharibu nchi zetu, ambapo watu wa mataifa haya mawili wanateseka kutokana na watu hawa wenye imani kali na magaidi.

Viongozi hao wawili wanaoungwa mkono na Marekani mara kwa mara wamekuwa wakilaumiana kwa kutofanya vya kutosha kuwadhibiti wapiganaji kutoka kila upande.