1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya wamuunga mkono Macron katika uchaguzi ujao

Bruce Amani
21 Aprili 2022

Viongozi wa siasa za wastani za mrengo wa kushoto wa Ujerumani, Uhispania na Ureno wamewahimiza wapiga kura wa Ufaransa kumchagua Rais Emmanuel Macron na sio mpinzani wake Marine Le Pen.

https://p.dw.com/p/4AFAo
Deutschland Berlin | Pedro Sanchez und Olaf Scholz
Picha: Filip Singer/REUTERS

Katika ujumbe wao uliochapishwa  kwenye magazeti kadhaa ya Ulaya, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez na Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa wameandika kuwa duru ya pili ya uchaguzi wa rais ni muhimu kwa Ufaransa na kila mmoja barani Ulaya.

Wamesema ni uchaguzi kati ya mgombea wa kidemokrasia anayeamini kuwa nguvu za Ufaransa zinatanuka katika Umoja wa Ulaya ulio na nguvu na uhuru na mgombea wa siasa kali anayewaunga mkono waziwazi wale wanaoushambulia uhuru na demokrasia na maadili.

soma zaidi: Macron aimarisha uongozi wake katika mjadala wa televisheni

Macron Rais wa siasa za mrengo wa wastani na Le Pen mpinzani wake wa siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia lwameanza mkondo wa mwisho wa kampeni kabla ya uchaguzi wa Jumapili.

Chanzo: afp