1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi waomboleza kifo cha Kofi Annan

19 Agosti 2018

Kutoka  katika bara lake la  Afrika hadi  Marekani, salamu za maombolezi zilimiminika  kutoka  kwa viongozi duniani  kote Jumapili, baada  ya Kofi Annan kufariki dunia.

https://p.dw.com/p/33NW8
UN Kofi Annan
Picha: Reuters/D. Sinyakov

Kiongozi huyo wa  Umoja  wa  mataifa na  mshindi  wa  tuzo ya amani  ya  Nobel, na  mwanadiplomasia  nyota, Kofi Annan alifariki akiwa  na  umri wa  miaka  80.

Raia  huyo  wa  Ghana alikuwa kazi  yake  ni  mwanadiplomasia ambaye  aliongoza  kwa  heba  ya  kimya  kimya  na  alipata  sifa sehemu  kubwa  kwa  kupandisha  hadhi  ya  taasisi  hiyo  kubwa  ya kimataifa   katika  siasa  za  dunia  wakati  wa  vipindi  viwili  akiwa mkuu  wa  Umoja  wa  mataifa  kuanzia  mwaka  1997  hadi  2006.

Katibu  mkuu  wa  kwanza  kutokea  katika  eneo  la  Afrika  kusini mwa  jangwa  la  Sahara, Annan  aliuongoza  Umoja  wa  Mataifa katika  miaka ya  mtengano  katika  vita  vya  Iraq na  baadaye alishutumiwa  kwa  rushwa  katika  kashfa  ya  mafuta  kwa  chakula , moja  kati  ya  nyakati  ngumu kabisa  katika  kipindi  chake  cha uongozi.

Familia imesema alifarikia kwa amani

Annan "kwa  ustadi  mkubwa  aliuongoza  Umoja  wa  mataifa  katika karne  ya  21 akielekeza  ajenda muhimu ambazo  ziliufanya  Umoja wa  mataifa  kuwa  na  mwelekeo  halisi  wa  amani, ufanisi na heshima  ya  utu duniani  kote," mrithi  wa  Annan  katibu  mkuu  wa Umoja  wa  Mataifa , Ban Ki-moon , alisema  katika  taarifa.

Belgien Kofi Annan und Condoleezza Rice
Annan akiwa na Condoleezza RicePicha: picture-alliance/ dpa/Y. Logghe

Familia  ya  Annan  ilisema  kwamba  alifariki  kwa  amani  siku  ya Jumamosi baada  ya  kuugua  kwa  muda  mfupi.

Annan , ambaye  aliishi  si  mbali  na  Umoja  wa  Mataifa  katika makao  yake  makuu  ya   Ulaya  mjini  Geneva, aifariki  hospitalini katika  eneo  linalozungumza  Kijerumani  la  nchi  hiyo, shirika  la habari  la  Uswisi ATS  limeripoti.

Katibu  mkuu  wa  sasa  Antonio Guterres  amemueleza  mtangulizi wake  huyo  kuwa, "ni nguvu  inayoelekeza kwa  ajili  ya  mambo mema".  "Katika  njia  nyingi , Kofi Annan alikuwa  Umoja  wa mataifa,"  alisema.

"Alipanda kupitia  ngazi  mbali  mbali  na  kuliongoza shirika  hilo katika  milenia  mpya kwa heshima  ambayo  haina  mfano na dhamira.

Desmond Tutu amesema Annan ni binadamu maarufu

Umoja  wa  Mataifa  umesema  utapepea  bendera  nusu  mlingoti katika  maeneo  yake  yote duniani  kote siku  ya  Jumanne.

Kofi Annan und Angela Merkel
Annan akiwa na Angela MerkelPicha: picture-alliance/dpa/F. Heyder

Na  rais  wa  Ghana Nana Akufo - Addo  alitangaza  wiki  ya maombolezo kwa kumkumbuka "mmoja  kati  ya raia mwenye hadhi ya  juu  kabisa".

Mwaka  2001, wakati  dunia  ikiwa katika  mtafaruku  wa  shambulio la  kigaidi  la  Septemba  11 nchini  Marekani, Annan  alipewa  tuzo ya  amani  ya  Nobel kwa  pamoja  na  taasisi  hiyo  ya  dunia "kwa kazi  yake kuiweka  dunia  kuwa  bora  na  iliyo  na  amani".

Mshindi  mwingine  wa  tuzo  ya  amani  ya  Nobel , askofu  mstaafu Desmond Tutu, amemueleza Annan  kuwa "ni binadamu maarufu ambaye  ameliwakilisha  bara  letu na  dunia kwa neema, heshima na  nidhamu.

Alizaliwa mjini  Kumasi, mji  mkuu  wa  jimbo  la  Ashanti  nchini Ghana, Annan  alifanyakazi  kwa  miongo  minne  katika  Umoja  wa mataifa na  alikuwa  mkuu  wa  kwanza  wa  taasisi hiyo  akitokea katika shirika  hilo.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / afpe
Mhariri: Jacob Safari