1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipi mtu huwa waziri Ujerumani ?

10 Februari 2009

Ujerumani imejipatia waziri mpya wa Uchumi.

https://p.dw.com/p/GqiU
Karl-Theodor zu Guttenberg )Picha: AP

Vipi mtu huwa waziri Ujerumani ? Swali hili limeiobuka kufuatia kujiuzulu hivi punde kwa waziri wa uchumiwa Ujerumani Bw.Michael Glos .Bw.Glos alichukua wadhifa wa waziri wa uchumi wa Ujerumani shingo upande hapo Novemba 2005.Sasa lakini ameutua mzigo huo kufuatia hali ya kutatanisha iliozuka serikalini mjini Berlin.

Kuparamia ngazi ya wadhifa wa uwaziri Ujerumani kuna njia moja tu-hii ni kwa muujibu wa mtaalamu wa sayansi ya kisiasa Gero Neugebauer kutoka Chuo Kikuu cha Berlin cha Free University :

"Mtu akitaka kuwa waziri nchini Ujerumani,lazima kwanza ajiunge na chama cha kisiasa au amependeza machoni mwa cghama fulani ili apendekezwe kushika uwaziri."

Mtaalamu mwenzake Wichard Woyke wa Chuo Kikuu cha Munster anaongeza:

"Unakuwa waziri tu kupitia chama cha kisiasa.Hii maana yake,mapatano ya kuunda serikali za muungano kati ya vyama, inasema vyama ndivyo vinavyoamua nani awe waziri na hakuna mwengine.Hii ni sawa isemavyo katiba ya shirikisho au ya serikali za mikoa kuwa, mkuu wa serikali huamua nani afaa kuwa waziri."

Ni kweli, kifungu cha 64 cha katiba ya Ujerumani-Grundgesetze kinasema waziri mtu huwa baada ya kupendekezwa na Kanzela (Waziri-mkuu) na kuidhinishwa na Rais na hata kupopkonywa wsadhifa huo.

Lakini katika ksa cha hivi sasa, chama cha mkoa wa bavaria cha CSU kimeamua nani Kanzela Angela Merkel amteue kuwa waziri mya wa uchumi.Aliechaguliwa ni Bw.Theodor zu Guttenmberg,mtu ambae hadi sasa akijishughulisha zaidi na siasa za nje.

Mtaalamu wa sayansi ya kisiasa Woyke anadai kwamba waziri anapaswa kuwa na uwezo na hekima ya kuongoza wizara kisiasa,lakini hii haina maana anabidi kila upande kuwa ujuzi wa shughuli za wizara anayiongoza.

Anaongeza,

Kuungwamkono chamani na katika mashina ya chini ya chama-ndio wilaya yake anayoegemea na kusimamia-panapozuka shaka shaka huwa ni turufu muhimu zaidi kuliko ujuzi wa fani ya wizara yake -kwa muujibu wa mtaalamu Neugebauer wa Chuo Kikuu cha Free University Berlin.

Anasema kuna matawi ya chama ya mikoani yanayoamua uwakilishi unaozingatia mikoa na ukubwa wake.Kwa kadiri tawi la chama lilivyo kubwa mikoani,ndipo huwa na sauti kubwa zaidi kuwakilishwa mkoa huo na waziri serikalini.

Kwa mfano, waziri wa ulinzi wa sasa Bw.Jung,amekuwa waziri wa ulinzi kwa kuwa mkoa wake wa Hessen unastahiki kutoa wadhifa wa uwaziri .

kimsingi, Bw, Jung ni mwanasheria ,sawa na waziri wa uchumi aliengatuka hivi punde Michael Glos,hakugangania kushika wadhifa huo.

Nchini Marekani,Rais Barack Obama, amemteua Steven Chu kuwa waziri wa nishati,mtaalamu wa fizikia asieegemea chama chochote.

Mtu anajua vipi Kanzela Angela Merkel akiwa nae mtaalamu wa fizikia, angelichagua Baraza lake la mawaziri laiti angelikuwa na uwezo wa kujiamulia atakavyo.