1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita dhidi ya Hamas

30 Desemba 2008

Nini mwishoe wa vita dhidi ya Hamas ?

https://p.dw.com/p/GPAF
Ehud Olmert na E.Barak(Israel)Picha: AP

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani yametuwama zaidi juu ya kupandishwa mno kwa bei ya gesi nchini na makampuni,vipi kukabiliana na wimbi la wakimbizi kutoka Afrika katika pwani ya Itali,lakini hasa vita vya Israel dhidi ya chama cha Hamas huko Mwambao wa Gaza.

Gazeti la Mannheimer Morgen juu ya wimbi la wakimbizi kutoka Afrika.Laandika:

Kuongeza kupiga doria katika pwani ya Libya kama anavyodai waziri mkuu wa Itali aliehemewa Silvio Berlusconi,sio jibu pekee linalotosha kupambana na tatizo hili la wakimbizi linalozidi kufadhahisha. Umoja wa Ulaya usitumbue zaidi macho na kuangalia vipi kila mwaka mamia ya wanadamu wanapoteza maisha yao baharini katika marekebu zilizosheheni .

Yule atakae kuzuwia wakimbizi waliokata tamaa ya maisha kutoka Nigeria, Mali au Somalia wasikimbilie Ulaya kutafuta maisha bora,anapaswa kuboresha hali za maisha huko huko nchini mwao wanakotoka.

Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul alikwishaonya kutopunguza misaada ya maendeleo katika wakati huu wa msukosuko...."

Likituchukua katika mzozo wa sasa wa Mashariki ya kati huko mwambao wa Gaza, gazeti la OSNABRUKA SEITUNG -Osnabruecker Zeitung lauliza:

Israel ina shabaha gani katika hujuma zake hizi kubwa-je, ni kukiteketeza chama cha Hamas kama vile viongozi mashuhuri wa Israel walivyonadi ?

Gazeti laendelea:

"Tujikumbushe kilichotokea majira ya kiangazi ya mwaka 2006.Wakati ule Israel iliazimia kukiteketeza chama cha Hizbollah nchini Lebanon.Matokeo yake Hizbollah leo ina nguvu zaidi kuliko hapo kabla. Hujuma ya sasa huko Gaza nayo italeta matokeo fulani ya msiba. Picha za mapigano majumbani na za watoto waliouwawa tena katika eneo la wasi wasi mkubwa na ambazo zaweza zikachochea moto mkubwa kuenea........."

Westdeutsche Zeitung kutoka Dusseldorf linahisi:

Pande zote mbili zina haki na hazina haki pia.Pale mtu anapoishambulia nyumba yako kwa maroketi,basi itakupasa kuilinda familia yako isidhurike.

Na ikiwa mtu atakuzingira kila upande usitoke na anakunyima kila nafasi ya kuwa na maisha bora ufanye nini ? basi pia utajilinda.Mwishoe lakini matokeo yake ni vita vinavyozaa vita."

Vita huko Gaza yamkini vikaleta ushindi kijeshi kwa Israel, kisiasa lakini,ladai Allgemeine Zeitung inazirejesha nyuma kwa miaka mingi juhudi zote za amani na kuishi pamoja Mashariki ya kati.Kwani, lasema gazeti,

"Kwa jicho la waislamu wengi duniani hapa dola kuwa la kidhalimu linawakanyaga na kuwaponda wapiganyaji majabari na wanaopigania haki yao.Kwahivyo, vita huko Gaza yamkini vikamalizikia tena kama vita vingi ambavyo Israel ilipigana:Vita imeshinda, utuluvu na amani upo mbali mno kuupata."