1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita kati ya Israel na Hamas vyaingia mwezi wa sita

Amina Mjahid
7 Aprili 2024

Vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas vimeingia mwezi wake wa 6, huku Marekani na wapatanishi wengine wakitarajiwa kujiunga na wenzao wengine mjini Cairo kujaribu kufikia makubaliano juu ya usitishwaji wa mapigano

https://p.dw.com/p/4eVw7
Ukanda wa Gaza
Mzozo kati ya Israel na Hamas waingia mwezi wa sia huku wapatanishi wakiendelea kutafuta njia za kusitisha mapiganoPicha: Jehad Alshrafi/Anadolu/picture alliance

Ujumbe wa Cairo pia utajadili hatua za kuachiwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika ukanda wa Gaza.

Kulingana na shirika la habari la Misri Al-Qahera, Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi, CIA, Bill Burns na Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al-Thani, watajiunga na ujumbe wa wapatanishi mjini Cairo na kuwa na mazungumzo ambayo sio ya moja kwa moja na maafisa wa Qatar na Hamas. 

Vita vya Gaza vinakaribia nusu mwaka, huku matumaini ya kumalizika yakiwa hayapo

Hamas ilithibitisha kwamba moja ya matakwa yake katika mazungumzo hayo ni kusitishwa kabisa mapigano mjini Gaza na wanajeshi wa Israel kuondoka huko.