1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Gaza-Israel

Eric Kalume Ponda7 Januari 2009

Jeshi la Israel limetangaza kuwa litasimamisha mashambulizi kwa muda wa masaa matatu kila siku .

https://p.dw.com/p/GTVS
Wanajeshi wa Israel wakiingia GazaPicha: AP


Tangazo hilo limetolewa huku mashambulizi makali yakiendelea usiku kucha kwa siku ya 12 mfululizo katika eneo hilo la Gaza.

Mashambulizi hayo ya leo yanaripotiwa kujibiwa vikali na wafuasi wa kundi la Hamas huku idadi ya waliofariki ikiendelea kuongezeka katika pande zote pimbili.

Akitoa tangazo hilo msemaji wa jeshi la Israel Avital Liebovich,alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa nafasi ya misaada ya humuda za kibinadamu kuwafikia wahanga wa mashambulizi hayo katika miji ya Gaza.

Avital Liebovich alisema kuwa, sasa jeshi la Israel litasimamisha mapigano kuanzia saa saba hadi saa kumi alasiri kila siku. ingawa hakutoa maelezo zaidi hatua hiyo itatekelezwa kwa muda gani.

Hatua hiyo imechukuliwa huku mashambulizi makali yakiripotiwa kuendelea katika miji ya eneo hilo la Gaza, iliyozingirwa na jeshi la Israel tangu mwanzoni mwa wiki hii, katika juhudi za kuwasaka wafuasi wa Hamas na maficho yao.

Serikali ya Israel inasema kuwa itaendelea na mashambulizi hayo, hadi pale itakapohakikisha kuwa uwezo wa wa kivita wa Hamas umeangamizwa kabisa.

Majeshi ya Israel yakitumia vifaru,yaliingia ndani ya mji wa Khani Yunis kwa siku ya pili sasa, ambapo watu watano waliuawa na wengine ambao idadi yao haikutolewa mara moja kujeruhiwa kwenyesha oparesheni hiyo iliyochukua muda wa masaa 24.

Mashambulizi hayo yameendelea licha ya jamii ya kimataifa kuitaka Israel kusitisha vita hivyo. Mawizi wa mashauri ya nchi za Nje wa Israel Tzipi Livni alisisitiza kuwa vita hivyi havikusudiwa raia wa Palestina na kwamba Israel haipasi kueleweka vibaya na jamii ya kimataifa.

Tzipi Livni alisema... ``Hivi ni vita dhidi ya ugaidi, na matarajio yetu kutoka jumuiya ya kimataifa ni kupeleka ujumbe unaostahili kwa magaidi ya kwamba hawatapewa au kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa, hususan kupitia umoja wa mataifa´´


Kwa upande wake Wafuasi wa Hamas yaripotiwa walirusha mizinga 30 ya Roketi usuki wa kuamkia leo dhidi ya maeneo ya Israel kujibu mashambulizi hayo ya Israel.

Hadi kufikia sasa watu wasiopungua 666 wameuliwa na wengine 2,950 kujeruhiwa katika upande wa Wapalestina.

Jumla ya Watoto 215 ni miongoni mwa waliouliwa tangu mashambulizi hayo yaanze mnamo tarehe 27 mwezi Disemba.

Hali imeendelea kuwa mbaya kwa wakaazi wengi wa eneo hilo la Gaza huku hospitali zikiendelea kukumbwa na hali ngumu kutokana na uhaba wa madawa na vifaa vingine vya matibabu.

Zaidi ya watu 48 waliuliwa katika shule moja inayoendeshwa na umoja wa Mataifa katika mji wa Jabiliya huku wito ukitolewa wa kufanywa uchunguzi zaidi kuhusiana na shambulio hilo.

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa kuhusiana na hali inayowakumba wakaazi 1.5 wa eneo la Gaza lenye wakaazi wengi.

Mjumbe wa umoja wa mataifa katika eneo hilo John Ging anasema kuwa jamii ya kimataifa inapasa kuchukua hatua za dharura katika kukomesha mauaji yanayoendelea Gaza.

Habari zaidi zinasema kuwa afisa wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Al-qaeda Anyman ametoa onyo kali kwa Israel akisema kuwa huenda vituo vyake vikashambuliwa mahali popote ulimwenguni.

Wafuasi wa Hamas imepuuzilia mbali wito wa jamii ya kimataifa ya kutambua taifa la Israel, kusitisha mashambulizi dhidi ya taifa hilo na kudumisha mkataba wa amani katika eneo hilo la Gaza.