1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi Chad watishia majeshi ya kulinda usalama

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVPL

NDJAMENA.Waasi nchini Chad wamesema kuwa majeshi yoyote ya kigeni yatakayopelekwa nchini humo kama sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Ulaya watatayachukulia kama adui.

Waasi hao wa Union of Forces for Democracy and Development UFDD wamesema kuwa wanajichukulia kuwa wako katika hali ya vita dhidi ya majeshi ya Ufaransa au mengine ya kigeni katika ardhi yao.

Majeshi ya Ufaransa pamoja na ndege za kijeshi tayari yameshakwenda Chad chini ya mwavuli wa mkataba wa amani.

Jeshi la Umoja wa Ulaya ambalo takriban nusu ni kutoka Ufaransa linatarajiwa kupelekwa katika eneo la karibu na mpaka na Sudan kuwalinda wakimbizi na wafanyakazi wa misaada.

Rais Nicolas Sarkozy alipuuza juu ya vitisho vya waasi hao na kusisitiza kuwa vitisho hivyo havitazuia upelekwaji wa kikosi hicho.