1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge 32 wa DRC wafariki tangu kuanza kwa janga

Tatu Karema
28 Mei 2021

Naibu spika wa bunge la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo asema wabunge 32 ama takriban asilimia 5 ya wabunge wote wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 tangu kuzuka kwa janga hilo

https://p.dw.com/p/3u7xQ
DR Kongo Präsident Felix Tshisekedi
Picha: Giscard Kusema/Präsidentschaftspresse der Demokratischen Republik Kongo

Hata baada ya Congo kama mataifa mengine ya Afrika kuripoti rasmi kuhusu idadi ndogo ya visa vya maambukizi ya corona na vifo, virusi hivyo vimewaathiri zaidi wabunge na msafara wa rais. Tangazo la hivi punde la serikali, limeripoti visa 31,248 vilivyothibitishwa na vifo 780 miongoni mwao wabunge 32. Haya ni kwa mujibu wa naibu spika wa bunge la nchi hiyo Jean-Marc Kabund.

Matamshi hayo yalitolewa kwa wabunge siku ya Alhamisi na Video kutolewa siku ya Ijumaa. Barakoa zinahitajika kuvaliwa ndani ya bunge lakini mara nyingi wabunge huingia bila kuzivaa na kukusanyika katika makundi makubwa na kupiga kelele kuwapongeza ama kuwazomea wasemaji.

Matukio ya kushangaza

Mnamo mwezi Desemba, wabunge na wengine waliokuwa ndani ya bunge walirushiana viti na ndoo wakati wa rabsha zilizosababishwa na mgongano kati ya Rais Felix Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila. Wengi walivaa barakoa zao chini ya videvu.

Tshisekedi alishangaza watu mapema mwezi huu wakati wa chakula cha jioni na wafuasi wake katika jiji la kusini mashariki la Kolwezi, aliposema kwa utani kwamba waliohudhuria walikuwa wakikiuka amri ya kutotoka nje iliyowekwa katika kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona na kusema, '' Leo muna ruhusa''.

Kukwama kwa mpango wa kutoa chanjo

Kampeni ya chanjo ya Congo imekwama baada ya kucheleweshwa kutolewa kwa chanjoi kwasababu ya wasiwasi wa usalama kuhusu chanjo ya AstraZeneca. Kutokana na hali hiyo, takriban asilimia 75 ya chanjo milioni 1.7 zilizopokelewa mnamo mwezi Machi ilibidi kuzigawanywa kwengineko ili kuwa na uhakika wa kutumika kabla ya kufikia muda wa mwisho wa matumizi yake.

WHO yakiri kutochukuwa hatua za haraka katika madai ya unyanyasaji wa kijinsia Congo

Schweiz Generaldirektor der Weltgesundheitsorganisation (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi mkuu wa WHO - Tedros Adhanom GhebreyesusPicha: Christopher Black/WHO/REUTERS

Wakati huo huo, Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amekiri kwamba shirika hilo halikuchukuwa hatua za haraka kuhusiana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia zinazohusu wafanyikazi ambao walifanya kazi nchini Congo wakati wa mripuko wa virusi vya Ebola kufuatia uchunguzi wa shirika la habari la Associated Press uliogundua kwamba maafisa wakuu wa shirika hilo la WHO walijuwa kuhusu visa kadhaa vya utovu wa nidhamu.

Huku baraza kuu la afya duniani likikutana wiki hii, mataifa yanashughulikia masuala kama jinsi ya kufanyia marekebisho mipango ya dharura ya shirika hilo la afya  baada ya kasoro zake katika kulishughulikia janga la virusi vya corona.

Baraza hilo halijaweka ajenda maalumu katika madai hayo ya ukosefu wa nidhamu nchini Congo lakini mkutano kuhusu kuzuia hujuma za kingono na dhulma unatarajiwa siku ya Ijumaa.

Hata hivyo wanasiploamasia wamemshinikiza  Ghebreyesus kuhusiana na swala hilo katika mkutano wa faragha. Wiki iliyopita, takriban mataifa sita yalielezea wasiwasi  kuhusu jinsi shirika hilo linavyoshughulikia dhulma za kijinsia na hujuma kwa kutaja ripoti za hivi karibuni za vyombo vya habari.