1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wa Barcelona kupunguziwa mishahara

27 Machi 2020

Klabu ya Barcelona imesema Ijumaa itapunguza mishahara ya wachezaji wake katika kipindi hiki ambacho ulimwengu unatikiswa na janga la Corona.

https://p.dw.com/p/3a8Op
UEFA Champions League | SSC Neapel - FC Barcelona | Fans Atemschutz Coronavirus
Picha: Getty Images/M. Steele

Kupitia bodi yake ya utendaji, klabu hiyo imeamua kusimamisha mikataba ya wachezaji wake kwa muda. Hata hivyo, klabu hiyo haijaweka wazi ni kwa kiwango gani mishahara hiyo itapunguzwa.

Nchini Uhispania, sheria zinaruhusu waajiri kupunguza gharama za kazi japo kwa kutoa hakikisho kuwa wafanyakazi watarudishwa kazini pindi tu mazingira ya kazi yatakapokuwa mazuri.

Visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vimepindukia hadi 7,800 kufikia Ijumaa na kufikisha idadi jumla ya watu walioambukizwa virusi hivyo kuwa 64,059 nchini Uhispania.

Vile vile, idadi jumla ya vifo vilivyotokana na Corona imefikia 4,858. Nchi hiyo ni ya pili barani Ulaya na ya nne duniani kwa kuongoza kwa idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya Corona.

Wizara ya afya nchini humo imesema kuwa karibu watu 10,000 waliokuwa wameambukizwa virusi hivyo wamepona.