1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wademokrat wakutana kujipanga upya

Admin.WagnerD24 Februari 2017

Chama cha Demokrat kikiwa hakiko tena madarakani kinatafuta njia za kusonga mbele kuimarisha nguvu za vuguvugu la upinzani ambao umenawiri tokea Rais Donald Trump aingie madarakani.

https://p.dw.com/p/2YC6L
US Demokraten
Picha: picture alliance/ZUMA Press/Katherine Clark's Office

Mkutano wa siku tatu wa chama hicho unaofanyika katika mji wa kusini wa Atlanta ambao unatazamiwa wabunge wapya  watakaochaguliwa wa chama hicho  kutunga sera ambazo zinatakiwa na vuguvugu hilo.

 

Kitu kinachofaa kwa chama hicho ni kuutumia mtandao unaotafutiana wa makundi ya waliberali na wapenda maendeleo kama msisimko uliozushwwa na matandao wa Facebook uliopelekea mandaamano ya nchi nzima ya wanawake siku moja baada ya kuapishwa kwa Trump kuwahimiza wapiga kura kushiriki katika uchaguzi wa magavana na uchaguzi maalum wa kamati za bunge mwaka huu pamoja na zile za kipindi cha kati za bunge hapo mwakani.

Chama cha Republikan kinadhibiti Ikulu,bunge na viti vya ugavana 33 na iwapo Neil Gorsuch anayependrekezwa na Trump kushika wadhiga wa jaji mkuu wa Mahakama Kuu atathibitishwa wahafidhina watakuwa na usemi katika mahakama kuu.

"Watu wa ngazi ya chini hawawezi kushinda bila ya kuwa na nguvu za kisiasa na wenye nguvu za kisiasa hawawezi kushinda bila ya kuwa na watu wa ngazi ya chini."  anasema hayo Brad Bauman mliberali ambaye ni mshauri elekezi wa chama cha Demokrat.Anasema kuna hali ya kutoaminiana hapo lakini itabidi wafikirie vipi hilo linaweza kushughulikiwa.

Nguvu ni umeme

USA Thomas Perez
Thomas Perez waziri wa zamani wa ajira anayewania uwenyekiti wa taifa chama cha Demokrat.Picha: Getty Images/C. Somodevilla

Wagombea wakuu wa wadhifa wa mwenyekiti mpya wa taifa wa chama hicho cha Demokrat wanasema wanakubaliana na jambo hilo."Nguvu ni umeme"  anasema hayo waziri wa zamani wa ajira Tom Perez ambaye anawania wadhifa huo wa juu wa chama pamoja na mbunge wa Minneasota na wengine.

Wagombea hao pamoja na watendaji wengine wakuu wa chama na viongozi wa makundi ya waliberali wanazungumzia juu ya jinsi ya kuliongezea nguvu vuguvugu dhidi ya Trump ambalo limeanza na maandamano ya mitaani mwezi uliopita na kuendelea wiki hii wakati wabunge wa chama cha Repubulika walipokabiliana na wapiga kura wao wenye ghadhabu katika manispaa za nchini kote Marekani.

Miongoni mwa makundi ya vuguvu ni pamoja na Black Lives Matter, Swing Left,Indivisible,Resist Trump Tuesdays ,Knock Every Door,Rise Stronger na Sister District

Hakuna kutofautiana 

US-Einreiseverbot gegen Muslime: Widerstand in den USA
Maandamano dhidi ya Trump mjini Boston katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani.Picha: Reuters/B. Snyder

Mwenyekiti wa chama cha Demokrat wa jimbo la Luosiana Karen Carter Paterson anasema mengi ya makundi hayo tayari yanawahusisha wanachama wengi wa Demokrat kwa hiyo hakuna kutofautiana hasa.

Anasema ni suala la chama kuchukuwa hatua zaidi kusaidia kuziunganisha juhudi zao,kusajili wagombea na kuwajuwa wapiga kura na wafanyakazi wa kujitolea. Mwanamke huyo anawania wadhifa katika kamati kuu ya chama cha Demokrat utakokuwa na jukumu la kuelekeza harakati za kiraia.

Kusajili wanachama wapya litakuwa jambo muhimu kwa chama hicho katika kipindi hiki cha baada ya enzi ya Obama na sio tu kwa ajili ya chaguzi za bunge bali pia kuelelekea Ikulu mwaka 2020.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AP

Mhariri:  Yusuf Saumu