1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili waisaidia Afghanstan

13 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/EJ3K
Mkutano wa wafadhili wa kuisaidia AfghanstanPicha: AP

Wafadhili kutoka nchi zaidi ya 80 na mashirika ya kimataifa wamekamilisha mkutano wao mjini Paris Ufaransa ambao ulidhamiriwa kuisaidia Afghanstan katika mpango wake wa miaka mitano wa kimaendeleo.

Wafadhili hao wa kimataifa wamechangisha dolla billioni 21 za kimarekani za kuisaidia nchi hiyo kuimarisha usalama na kuwalisha watu wake maskini wanaohitaji kwa haraka msaada huo.

Mkutano huo wa wafadhili uliomalizika mjini Paris umeahidi zaidi ya dolla billioni 20 zitakazotumika kusaidia ujenzi mpya wa Afghanstan nchi ambayo inakabiliwa na mapigano ya wanajeshi wa jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi Nato na wanamgambo wa kitaliban.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernerd Kouchner amesema mchango huo wa wafadhili ni mafanikio makubwa kwa sababu kiasi kilichotolewa ni cha kutia moyo.

Rais Karzai wa Afghanstan aliwatolea mwito wafadhili kugharamia sehemu ya mpango wa kimaendeleo wa nchi yake ambao unahitaji dollah billioni 50 za kupambana na umaskini uliokithiri pamoja na wanamgambo wakitaliban katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano ijayo.

Mchango mkubwa umetolewa na Marekani ambapo mke wa rais Bush bi Laura Bush aliahidi msaada wa dolla billioni 10.2 katika kipindi cha miaka 2 ijayo.

Uingereza pia imeahidi kutoa dolla bilioni 1.2 katika kipindi cha miaka mitano ijayo wakati Japan ikitangaza ahadi ya kutoa dolla millioni 550 huku Ujerumani ikisema itatoa zaidi ya euro 420 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir akizungumza kwenye mkutano huo wa Paris ametilia mkazo wa kuendelezwa juhudi za pamoja katika jumuiya ya NATO kuisadia Afghanstan kukabiliana na wanamgambo wakitaliban.Akaongeza kusema tukimnukulu.

''Ninavyodhani mimi sio kusimamisha juhudi zetu za pamoja nchini Afghantan na kuwaachia waafghansta mzigo kuubeba wenyewe,ni kinyume chake.''

Kwa upande mwingine wafadhili wamemtolea mwito rais Karzai kutia juhudi zaidi za kupamabana na rushwa pamoja na kuimarisha utawala wa kisheria katika nchi yake ambayo imesambaratishwa na umaskini na mapambano ya mataliban.

Rais Karzai fedha zilizotolewa zitatumiwa kuwapiga jeki wakulima na kuwafanya kuondokana kwa kiasi na utegemezi wa biashara ya kilimo cha kasumba na madawa ya kulevya. Suala la ulinzi ambalo ni muhimu kwa sasa nchini humo pia limejadiliwa ambapo waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Joseph Jung akigusia juu ya kuimarishwa mchango wa kijeshi wa Ujerumani nchini Afghanstan alisema.

''Nimeweka wazi kabisa kuwa kabla ya likizo ya majira ya jiangazi yajayo ntaarifiwa na insepekta mkuu wa jeshi la nato juu ya kile nnachohisi mimi kinahitajika kuhusiana na jukumu jipya la jeshi la Ujerumani nchini Afghanstan.''

Mapambano dhidi ya waasi nchini Afghanstna ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali ya nchi hiyo na jumuiya ya kimataifa ili kuleta usalama na utengamano nchini humo.

►◄