1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina waongoza katika uchaguzi wa Iran

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOsW

TEHRAN:

Ripoti za mwanzo juu ya uchaguzi wa bunge uliofanywa siku ya Ijumaa nchini Iran,zaonyesha kuwa wahafidhina wenye msimamo mkali wanaongoza.Wapendao mageuzi pia wamepata viti kadhaa katika miji ambako waliruhusiwa kugombea uchaguzi huo.

Takriban nusu ya wapinzani wa Rais Mahmoud Ahmedinejad alie na msimamo mkali wa kihafidhina,walipigwa marufuku kushiriki katika uchaguzi wa jana.Wapendao mageuzi walitumaini kunufaika kutokana na hali ya kutoridhika miongoni mwa wananchi wengi kwa sababu ya ughali wa maisha ulioongezeka kwa asilimia 19.Lakini wajumbe wengi wanaounga mkono mageuzi hawakuruhusiwa kugombea uchaguzi.