1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji na ujuzi wao katika nchi tajiri

21 Februari 2008

Nchi tajiri zimetakiwa kuchukua hatua zaidi kuwajumuisha wageni katika jamii zao pamoja na kuwapatia ajira, ikiwa kweli zinataka kuwa na tija za kiuchumi kutokana na ujuzi na uwezo wa wahamiaji.

https://p.dw.com/p/DBCL
Baadhi wa wahamiaji katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin.Picha: DW

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD) iliotolewa mjini Paris.

Takriban katika nchi zote za ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, kundi la nchi 30 tajiri,wahamiaji wanajikuta zaidi wakifanya kazi katika maeneo ambako ujuzi wao binafsi ni mkubwa zaidi kuliko kazi zenyewe.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo, watafiti wa masuala ya uhamiaji na soko la ajira waTakriban katika nchi zote za jumuiya ya ikusanya takwimu kuhusiana na wahamiaji katika nchi wanachama. Kwa kila nchi miongoni mwa 30 zinazounda jumuiya hiyo, waliwatenganisha wahamiaji kutokana na nchi zao za asili, umri, viwango vya elimu, kazi na sekta wanayo shughulika nayo.

Mhamiaji ametambulishwa kama " mtu ambaye mahala alikozaliwa kunatafautiana na nchi anakoishi sasa." Kizazi cha pili cha wahamiaji na matatizo wanayokabiliana nayo ni suala linaloangukia nje ya mtazamo wa ripoti hiyo, iliopewa jina" Hali ya wakaazi wahamiaji katika karne ya 21."

Ripoti hiyo inasema kwamba idadi ya walio na elimu nyongeza baaada ya ile ya sekondari katika nchi wanachama wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, ni ya juu miongoni mwa wageni waliozaliwa nje kwa kiwango cha 24 asili mia, kuliko wenyeji ambacho ni 19 ,1 asili mia. Lakini pia idadi ya wageni wasio na elimu au kiwango cha jioni kabisa cha elimu ni kubwa miongoni mwa wageni kuliko wenyeji.

Wahamiaji wa hivi karibuni zaidi wanaelekea kuwa na elimu nzuri kuliko waliotangulia hapo kabla. Ujuzi wa hali ya juu unatokana na Wachina na Wahindi wanaohamia Marekani wanaotoka Asia wakitawala katika sekata za ufundi wa kimambo leo na sayansi.

Nchini Ugiriki, Italia na Uhispania, wanaofanya kazi ambazo wanaujuzi mkubwa nazo ni maradufu kuliko wafanyakazi wazawa.

Huenda wahamiaji wakawa na matatizo ya lugha na huenada wakahitaji muda kukabiliana na vikwazo vya kisheria na kiutawala -inasema ripoti hiyo. Wanaonyesha kuwa tayari kufanya kazi za chini wakitumai kupanda ngazi hapo baadae.

Kwa upande mwengine ripoti ya jumuiya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo, inasema kile kinachojulikana kama kuhama kwa wenye ujuzi na kuhamia n´gambo ni jambo linalo ziathiri zaidi nchi changa za Afrika na Caribbean. Nchi kama Jamaica, Mauritius na Fiji zina zaidi ya 40 asili mia ya watu wao wenye ujuzi nchi za nje. Nchini Msumbiji, Angola , Sierra Leone na Tanzanaia, au Tridnidad na Tobago kiwango cha wenye ujuzi wanaohamia nchi nyengine katika sekta ya afya kimefikia 50 asili mia.

Kwa upande wa Brazil, China na India, nchi hizo zina kiwango cha chini ya 5 asili mia ya wafanyakazi wao wenye ujuzi waliohamia n´gambo .

Bila shaka sababu kubwa ni kwamba nchi wanakoelekea , zinatoa nafasi zaidi za kimaisha na masilahi ni bora zaidi.

Nchini Marekani zaidi ya 20 asili mia ya waliozaliwa Asia wanafanyakazi nchini humo kama watalaamu katika sekta ya sayansi.

Kwa jumla Marekani ndiyo inayopokea wahamiaji zaidi ikiwa na wahamiaji wapatao 31.4 milioni kuanzia umri wa miaka 15 na kuendelea.

Nafasi ya pili ni Ujerumani ikiwa na karibu wakaazi milioni 8 waliozaliwa nchi za nje. Inafuatiwa na Ufaransa, Canada na Uingereza.