1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahusika wa mashambulio ya mabomu wasakwa India

27 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EkgA

AHMEDABAD

Maafisa wa polisi nchini India wanawasaka wahusika wa mashambulio ya mabomu yaliyofanywa katika mji wa Ahmedabad ambapo watu zaidi ya 40 waliuwawa na wengine wengi wakajeruhiwa.

Vyombo vya habari nchini India vimeripoti kwamba kundi lisilomaarufu linalojiita Mujaheedin katika India limedai kuhusika na mashambulio hayo.Hata hivyo serikali imewaonya kwamba mtu yoyote asitumie tukio hilo kuzusha hali ya wasiwasi zaidi miongoni mwa wananchi wa India.

Jana mashambulio 16 ya mambomu yaliyfanywa katika maeneo kadhaa ya India.Ahmedabad mji mkuu wa jimbo la Gujarat ni eneo kulikotokea ghasia mbaya ambapo wahindu waliwashambulia waislamu na maelfu ya watu wakauwawa mwaka 2002.

Ijumaa mashambulio saba madogo ya mabomu yaliukumbuka mji wa Bangalore na watu wawili waliuwawa.

Serikali ya India imetangaza hali ya tahadhari hii leo huku kukiwa na hofu ya mashambulio zaidi.

Wakati huohuo serikali imesema inashuku mashambulio hayo ya mabomu yamefanywa na makundi kutoka Pakistan na Bangladesh.