1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu washerehekea Eid el-Hajj

12 Septemba 2016

Waislamu ulimwenguni kote wanasherehekea sikuukuu ya Eid Ul Hajj. Mahujaji wamefika Mina leo Jumatatu(12.09.2016) kwa kutekeleza utaratibu wa kumpiga mawe shetani,kaida ya mwisho kuu ya Hijja ya kila mwaka.

https://p.dw.com/p/1K0Ty
Saudi-Arabien Hadsch - PilgerInnen in Mekka
Mamia kwa maelfu ya mahujaji wakitekeleza Hijja katika mlima ArafatPicha: Reuters/A. Jadallah

Eneo hilo hata hivyo lilitokea mkanyagano na kusababisha maafa makubwa mwaka jana.

Utaratibu wa kupiga mawe shetani unafanywa mara tatu katika muda wa siku zijazo.

Saudi Arabien Mekka Pilger Werfen der Steine auf die 'Aqaba-Säule
Mahujaji wakutupa vijiwe kuashiria kupiga mawe shetaniPicha: Getty Images/AFP/B. Mehri

Mara ya kwanza inakuja mwanzoni mwa sikukuu ya Eid l-Adha, ambayo ni leo siku ya kuchinja, siku ambayo ni takatifu kwa Waislamu, siku inayoadhimishwa na zaidi ya Waislamu bilioni 1.5 duniani kote.

Hatua kadhaa za usalama zimechukuliwa kuepusha kutokea tena kwa maafa yaliyotokea mwaka jana, ambayo yalisababisha kiasi ya watu 2,300 kufariki wakati wakiingia katika daraja la Jamarat kutekeleza kaida hiyo ya kurusha vijiwe kama ishara ya kumpiga shetani, tukio linalofuatia hatua ya nabii Ibrahim kumpiga vijiwe shetani wakati akimtaka asitekeleze amri ya Mwenyezi Mungu ya kumchinja mwanawe Ismail.

Saudi Arabien Mekka Pilger Kaaba
Al-Kaaba , mahujaji wakizunguka al-Kaaba mjini MakkaPicha: picture alliance/AP Photo/N. El-Mofty

Daraja hilo ni la ghorofa kadha ili kuweza kuwawezesha mahujaji wengi iwezekanvyo kutekeleza utaratibu huo, ambapo zaidi ya mahijaji milioni 1.8 wameshiriki mwaka huu.

Mahujaji hutupa vijiwe walivyovikusanya kutoka katika eneo la karibu la Muzdalifah siku ya Jumapili jioni dhidi ya kuta zilizojengwa kuwa kama ishara ya shetani.

Usalama waimarishwa

Mfalme wa Saudi Arabia Salman aliwasili Mina siku ya Jumapili kuhakikisha mahujaji wanatekeleza kaida hiyo "bila matatizo, kwa utulivu na usalama", shirika rasmi la habari la Saudia liliripoti.

Saudi Arabien Mekka Pilger Haare schneiden Hadsch Tamattu‘
Baadhi ya mahujaji wakinyoa nywele moja ya utaratibu wa HijjaPicha: Getty Images/AFP/M. Fala'ah

Pia alifahamishwa kuhusiana na matayarisho kwa ajili ya mahujaji kupita kwa usalama kati ya Muzdalifah na Mina.

Baada ya kumrushia vijiwe shetani , kondoo huchinjwa na nyama kugawiwa kwa Waislamu ambao hawana uwezo na masikini, ikionesha kuwapo tayari kwa nabii Ibrahim kumtoa mwanae Ismail kwa amri ya Mwenyezi Mungu amchinje, ambapo baadaye alitolewa kondoo badala ya kijana huyo katika dakika ya mwisho.

Kaida ya kutupa vijiwe inafuatia hatua za nabii Ibrahim kukataa vishawishi vya kutomtii Mwenyezi Mungu kutoka kwa shetani.

Saudi Arabien Mekka Pilger Berg Arafat
Mahujaji wakipanda mlima ArafatPicha: picture alliance/dpa/Y. Arhab

Mkanyagano na maafa

Mkandagano wa mwaka jana ulikuwa mbaya mno katika historia ya Hijja.

Saudi Arabia inaendelea kusisitiza kwamba watu waliofariki ni 769, lakini tarakimu zilizokusanywa kutoka kwa maafisa katika zaidi ya nchi 30 zinatoa idadi ya juu mara tatu zaidi.

Maafisa wametangaza kuanzisha uchunguzi kuhusiana na maafa hayo lakini hakuna kilichotangazwa hadi sasa kutokana na uchunguzi huo. Hatua kadhaa za usalama zimeanzishwa mwaka huu.

Saudi-Arabien Hadsch - PilgerInnen in Mekka
Mahujaji wakikusanyika katika mlima Arafat kabla ya kwenda MinaPicha: Reuters/A. Jadallah

Miongoni mwa hizo ni kuanzisha utaratibu wa kuvaa bangili maalum, ambayo huhifadhi data za binafsi za kila hujaji. Barabara pia zimepanuliwa katika eneo la Jamarat, magazeti ya nchi hiyo yameripoti.

Lakini hatua hizo mpya za usalama zilishindwa kuridhisha mahujaji wa kishia kutoka Iran , nchi ambayo ilikasirishwa mno na maafa hayo kwa kuwa ilipoteza mahujaji wengi katika mkasa huo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Yusuf , Saumu