1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakazi waliokimbia Volcano DRC watakiwa kurejea nyumbani

Admin.WagnerD7 Juni 2021

Mamia ya wakaazi wa Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo waliokimbia mlipuko wa volkano tarehe 22 ya mwezi Mei wametakiwa kuanza kurejea kwenye makaazi yao.

https://p.dw.com/p/3uY30
DRK Jean-Michel Sama Lukonde
Picha: Giscard Kusema/Press Office Presidency DRC

Mamia ya wakaazi wa Goma, katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliokimbia mlipuko wa volkano tarehe 22 ya mwezi Mei wametakiwa kuanza kurejea kwenye makaazi yao wakati huu ambapo serikali nchini humo kupitia waziri mkuu aliyeko ziarani mjini Goma imetangaza utulivu kwenye Mlima Niyaragongo ambao sio tena kitisho kwa wananchi wa eneo hilo. 

Waziri mkuu Jean Michel Sama Lukonde ametangaza hayo hii alipozungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini  Goma majuma mawili baada ya mlipuko wa volkano uliosababisha maelfu ya wananchi kuyakimbia makaazi yao.

Hata hivyo, kiongozi huyo aliyehitimisha ziara yake hii leo (Jumatatu) na ambaye ameelekea katika mkoa jirani wa Kivu Kusini amewataka wakazi kurejea majumbani kwao na kwamba hali ya kwenye mlima wa moto wa Nyiragongo kwa sasa ni tulivu.

Bildergalerie | DR Congo | Ausbruch des Nyiragongo und Evakuierung von Goma
Wakazi wakikimbia makaazi yao baada ya mlipuko huo uliotishia maisha yao.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Akisindikizwa na mawaziri wengi wa serikali kuu, amesema kuwa serikali ya Kongo itaanzisha hivi karibuni kazi za uchimbaji wa gesi katika Ziwa Kivu ambyo pia ni kitisho kikubwa kwa wakaazi wanaopakana na ziwa hili. Mlipuko wa volkano wa tarehe 22 Mei uliwafanya zaidi ya watu laki nne kuyahama makazi yao na nyumba kadhaa kuteketea kwa moto.

Mbele ya waandishi habari Lukonde ameyataka makundi yanaomiliki silaha kimagendo kujisalimisha na kuingia katika maisha ya kawaida.

Tofauti na awali ambamo wanamgambo walikua wakiingizwa katika jeshi zoezi ambalo lilionekana kuwa chanzo kikubwa cha machafuko yanaoendelea hapa nchini Kongo. Tangu mapema asubuhi  serikali hapa Kivu ya Kaskazini imenza kuandaa mabasi kwa ajili ya kuwaondoa maelfu ya wakaazi waliokimbilia katika maeneo mbalimbali kote hapa mashariki ya Congo.

Soma Zaidi: Goma yakabiliwa na uhaba wa chakula baada ya volkano

Benjamin Kasembe- Goma