1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

010710 First Ladies Deutschland

Sekione Kitojo2 Julai 2010

Kuwa mke wa rais nchini Ujerumani, sio kazi na kwa hiyo suala hilo halitajwi katika katiba ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/O9V2
"Mama wa kwanza wa taifa" Bettina Wulff akimbusu mumewe Christian Wulff mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Ujerumani.Picha: AP

Kuwa  mke  wa  rais  wa  Ujerumani , sio  kazi  na  kwa hiyo  suala  hilo  halitajwi   katika  katiba  ya  Ujerumani. Lakini  ni  jukumu, ambalo  linapaswa  kuangaliwa  kwa undani. Bettina Wulff ni, "mama  wa  kwanza  wa  taifa" wa  kumi, katika  historia  ya  jamhuri  ya  Ujerumani. Akiwa na  Christian Wulff, pamoja  na  mtoto  wao   wa  kiume mwenye  umri  wa  miaka  miwili pamoja  na  mtoto  kutoka katika  ndoa yake  ya  zamani  watahamia  katika  makaazi ya  kasri  la  Bellevue,  mahali  wanapoishi  marais.

Anataka  kuwa  kama  afisa  habari, ikiwa  ndio   wajibu wake  katika  wakati  rais  mume  wake atakapotumikia wadhifa  wake. Mshukuru mkeo kwa kuwa amekufanyia mengi.

Rais  wa  zamani  wa   Ujerumani  Horst  Köhler amekwishafanya  hivyo. Baada  ya  kuchaguliwa  kwake mwaka  jana  alimshukuru  hadharani  mkewe  Eva Luise Köhler. Familia  ya  Köhler  ilikuwa  ni  familia  iliyokuwa  na uhusiano  wa  karibu  sana, ikiwa  mkewe  ni  mtu  wa karibu  sana  anayempa  ushauri.

Mwamamume  huwa  imara  pale  anapokuwa  na  mke imara.

Mama  wa  kwanza  wa  taifa   Bettina  Wulff  anataka kuchukua  mfano  wa  aina  ya  Eva Köhlers, wa kuwakaribia  watu, na  kujishughulisha  katika  masuala  ya kijamii. Amesomea  masomo  ya  uhusiano  na  umma na akiwa  na  umri  wa  miaka  36,  Bibi  Bettina  Wulff anakuwa  mke  wa  kwanza  wa  rais  ambaye  ni  kijana zaidi  na  analeta  haiba  katika  kasri  la  Bellevue. Aina  ya maisha  yake  ya  mcheza  sinema  pamoja  na  michoro  ya tatoo  katika  sehemu  ya  juu  ya   mkono  wake imemfanya  aandikwe  katika  magazeti  kadha.

Bettina  Wulff  pia  hujishughulisha  na  masuala  ya kijamii. Hali  hii  inamuweka  karibu  na  wake  wa  marais waliopita. Wote  walijihusisha  na  huduma  za  kijamii  kwa ajili  ya  afya  ya  kina  mama  na  mtoto. Muasisi  alikuwa mke  wa  rais  wa  kwanza   wa  Ujerumani  Theodor Heuss, ambaye  alikuwa  akijihusisha  pia  na  masuala  ya  kisiasa na  mageuzi  ya  kijamii  Elly Heuss-Knapp katika  mwaka 1950.

Christina  Rau,  mke  wa  rais  wa  zamani  Johannes  Rau , alikuwa  pia  akishughulika   kama   alivyokuwa  akifanya bibi  yake, ambaye  alikuwa   ameolewa  na   rais  wa zamani  Gustav  Heinemann.

Nimeijua  jumuiya  hii   kupitia  bibi  yangu  Hilda Heinemann, ambaye  alikuwa  pia  kiongozi  ,  kwakuwa kulikuwa  na   aina  ya  utamaduni, kwamba   mke  wa  rais ni  lazima  awe  kiongozi  wa  jumuiya  hiyo.

Katika  mwaka  2000, katika  maadhimisho  ya  miaka  50 ya  jumuiya  hiyo  inayojishughulisha  na  kuwapa mapumziko  wanawake, anasema  Christina  Rau kumekuwa  na  ugawanaji  majukumu  baina  ya  wanaume na  wanawake.

Mzigo  mkubwa uliendelea  kubakia  kwa  akina  mama. Hali  hiyo  imebadilika  kidogo  hata  hivyo, lakini  takwimu zinaonyesha , kwamba  wakati  mtoto  wa  kwanza anapopatikana, kazi  alizokuwa  akifanya  baba   nyumbani zinaanza kupungua.  Ile  ndoto , kwamba  hakutakuwa  na sababu  ya  kuwapatia  mama  na  mtoto  uangalizi, kwa kuwa  mwenza  wake  atakuwa  anagawana  nae majukumu  ya  nyumba  kwa  kiwango  sawa,  hali  hiyo bado  iko  mbali  kabisa.

Na  katika  upande  wa  familia  ya   rais, ? Veronica Carstens  na  mume  wake  rais  wa  Ujerumani  Karl Castens  hawakuwa  na  mtoto. Veronica  Carstens  alikuwa akimsindikiza   mume  wake  kuanzia  mwaka  1979 anapokwenda  ziara  za  nje  na  katika  matukio  muhimu lakini  pia  alikuwa  anaendesha  shughuli  zake  za udaktari.

Mwandishi : Grunau, Andrea / ZR / Kitojo Sekione

Mhariri:Josephat Charo