1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakenya wanasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChHG

NAIROBI

Wananchi wa Kenya leo wanasubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hapo jana.

Matokeo yasio rasmi leo hii yanaonyesha Rais Mwai Kibaki wa Kenya akiwa kwenye mchuano mkali na mpinzani wake mkuu Raila Odinga kufuatia uchaguzi uliosifiwa kuwa wa utulivu licha ya vurugu za hapa na pale na shutuma za hujuma za uchaguzi kutoka pande zote mbili serikali na upinzani.

Wakari kura zikiendelea kuhesabiwa pole pole na hakuna matokeo rasmi yaliotolewa na maafisa wa tume ya uchaguzi Taasisi ya Elimu na Demokrasia shirika lisilo la kiserikali linaloheshimiwa limempa Kibaki asili mia 50.3 dhidi ya asili mia 40.6 kwa Odinga lakini takwimu hizo zinazingatia vituo 309 kati ya vituo 27,000 vya kupigia kura.

Vituo vikuu vya televisheni nchini Kenya matokeo yake yamegawika kwa kuzingatia hesabu za takriban kura 200,000 kituo cha NTV na Citizen vimesema Odinga anaongoza wakati KTN kimesema Kibali alikuwa mbele.

Wakenya milioni 14 walikuwa na haki ya kupiga kura lakini inategemewa kwamba wale waliojitokeza hasa kupiga kura ni kama milioni nane hadi kumi hivi.