1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakenya watamba mita 800 na 1.500

23 Agosti 2008

Olimpik Kenenisa bekele atwaa medali ya pili ya dhahabu mita 5000 -wakenya Bungei na Nancy Lagat katika mita 800 na 1.500.

https://p.dw.com/p/F3bY

Michezo ya 29 ya olimpik ya Beijing ikibakisha siku 1 kabla kufungwa rasmi hapo kesho,ilikua siku ya Kenya kutamba tangu katika mita 800 hadi mita 1.500.Muethiopia Kennenisa Bekele amemuigiza mwenzake Turnesh Dibaba na kuwa mwanariadha wapili wa Ethiopia tangu Miruz Yifter katika michezo ya Moscow kutamba katika mita 5000 na 10.000 hivi punde.Sabina Spitz ametwaa medali ya dhahabu kwa Ujerumani.

Mabingwa wapya wa olimpik wa dimba si Nigeria, bali Argentina iliikomea Nigeria leo bao 1:0 na kutwaa medali ya dhahabu.

Kesho ni mbio za marathon za wanaume-je,mkenya Martin Lel atatamba ? Tunazungumza na Cathrine Ndereba ,bingwa wa dunia wa marathon alienyakua medali ya fedha mara hii huko Beijing.

Leo ilikua siku ya wakenya katika finali ya mita 800 wanaume,mita 1500 wanawake na ya Ethiopia katika mita 5000 wanaume ambamo Kenenisa Bekele alitamba mbele ya bingwa wa dunia wa zamani na wa sasa -Eluid kipchoge wa Kenya na Bernhard Lagat,mzaliwa wa kenya aliekimbia kwa tiketi ya Marekani: Wilfred Bungei wa kenya ametawazwa bingwa wa olimpik wa mita 800,mkenya wa kwanza kuvaa taji hilo upande wa wanaume tangu michezo ya Barcelona, 1992.Alishika usukani na mapema na mwishoe akashinda kwa muda wa dakika 1:44.65.Ismail Ahmed wa Sudan alichukua medali ya fedha huku bingwa wa dunia mkenya Afred Kirwa Yego akiridhika na medali ya shaba.

Baadae ikawa zamu ya msichana wa Kenya Nancy Jebet kutoroka na medali nyengine ya dhahabu katika mita 1.500.Muda wake ulikuwa dakika 4.00.23.Muukraine Iryna Lishchnska alimaliza wapili huku mwenzake Nataliya Tobias akitwaa medali ya shaba.

Msisimko ulikua katika mita 5000 pale Kenenisa Bekele akifukuzwa na wakenya Eluid kipchoge na Edwin Soi waliobidi kuridhika na medali za fedha na shaba.Bekele alinyakua ushindi kwa muda wake wa dakika 12: na sek.57-rekodi mpya ya Olimpik. hii imekuwa medali ya 4 ya dhahabu kwa Ethiopia.Kenya pia ina medali 4 za dhahabu lakini nyingi zaidi za fedha kuliko Ethiopia.

Mjamaica Usain Bolt,bingwa wa olimpik na rekodi za dunia katika mita 100 na 200 alitamba tena katika mbio za mita 100X4 kupokezana na kutia jana mfukoni medali yake ya 3 ya dhahabu na medali zote 3 alizonyakua zimemalizikia rekodi ya dunia.Mwishoe,Bolt alinukuliwa kusema,"Ninachoweza kusema tu ni hiki-wendambio fupi za kasi wajamaica zinatawala dunia."

Kesho ni changamoto ya mbio za marathon wanaume:

Macho ya Afrika yatawakodolea wanariadha wa Kenya na Ethiopia.bingwa wa rekodi ya dunia muethiopia Haile Gebreselassie, bingwa wa rekodi ya dunia hayumo,kwani alijitoa kutokana na hali ya hewa ya Beijing.

Taji la marathon la wanawake lilikwenda Rumania.Kenya lakini iliondokea na medali ya fedha pale bingwa wake wa dunia -Cathrine Ndereba alipomaliza wapili :

Dimba la olimpik:

Nigeria, mabingwa wa olimpik wa dimba huko Atlanta,1996 waliondoka uwanjani leo na huzuni kwa uzembe waliofanya wa kutotia mabao kutoka nafasi nyingi walizopata.Ingawa ni wao waliotamba, mwishoe alilukua Lionel Messi na wenzake akina Juan Roman Riquelme walioshangiria ushindi wa medali ya dhahabu.Nigeria,ilibidi leo kuridhika na ile ya fedha.Brazil iliondoka juzi na medali ya shaba.

Michezo ya 29 ya olimpik inamalizika rasmi kesho kwa shangwe na shamra shamra kama ilivyoanza August 8-8-2008 -siku ya bahati njema kwa china:

China kweli imeangukiwa na bahati,kwani masaa 24 kabla pazia la michezo ya beijing kufungwa rasmi,China inaongoza kileleni mwa ngazi ya medali:Ina jumla ya medali 47 za dhahabu kwa 31 za mahasimu wao Marekani huku Uingereza ikiangukia nafasi ya 3 kwa medali zake 18.

Barani Afrika Ethiopia inaongoza kwa medali 4 za dhahabu ikifuatwa na Kenya.