1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi mashariki mwa DRC wapata msaada kutoka Ujerumani

19 Septemba 2013

Wakimbizi mashariki mwa Kongo kutoka vijiji vya Kamango na Mamundioma, katika wilaya ya Beni, wamepata msaada kwa mara ya kwanza kabisa, tangu vurugu zitokee katika maeneo ya Kamango, kaskazini mashariki mwa mji wa Beni.

https://p.dw.com/p/19kVR
Kambi ya Wakimbizi mashariki mwa Kongo
Kambi ya Wakimbizi mashariki mwa KongoPicha: AP

Wakimbizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka vijiji vya Kamango na Mamundioma, katika wilaya ya Beni, wamepokea msaada kwa mara ya kwanza kabisa, tangu vurugu zitokee katika maeneo ya Kamango, kaskazini mashariki mwa mji wa Beni.


Familia elfu Mbili na mia saba zinanufaika na msaada wa vyakula, vifaa vya matumizi ya nyumbani pamoja na mavazi kutoka shirika la msaada la Kijerumani Diakonie Katastrophen Hilfe, pamoja na serikali ya Ujerumani kupitia wizara yake ya mambo ya nchi za nje. Mwandishi wetu John Kanyunyu na habari kamili kutoka Beni. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Josephat Charo