1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walimwengu wasubiri kuijua hatima ya Brexit

Oumilkheir Hamidou
12 Machi 2019

Wabunge wa Uingereza watakabiliana na kizungumkuti cha ama kuunga mkono makubaliano yaliyofikiwa na waziri mkuu Theresa May au kuyapinga na kwa namna hiyo kuhatarisha zoezi lenyewe hasa la Brexit.

https://p.dw.com/p/3EqUr
Frankreich Brexit l Theresa May trifft sich mit Juncker in Straßburg
Picha: picture alliance/AP Photo/V. Kessler

Waengereza wanakabiliana na siku ya siku pale bunge lao litakapoyapigia kura makubaliano yaliyofikiwa na waziri mkuu Theresa May, aliyetamka siku moja kabla amefanikiwa kufikia maridhiano pamoja na viongozi wa Umoja wa ulaya mjini Strasbourg kuhusu kifungu kinachohusiana na mpaka kati ya Ireland ya kaskazini na jamhuri ya Ireland au Backstop. Pande hizo mbili, Theresa May na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker wakatangaza "marekebisho yanayodhaminiwa kisheria" ya mkataba wa awali ili kukidhi madai ya waingereza na kwa namna hiyo kufungua njia ya kuungwa mkono bungeni.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May akihutubia bungeni
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa Mayakihutubia bungeniPicha: picture-alliance/PA Wire/House of Commons

Wabunge wahimizwa waunge mkono makubaliano ya Brexit

Wakati  umewadia wa kukusanyika na kuunga mkono makubaliano yaliyofanyiwa marekebisho" amesema waziri mkuu Theresa May. Na waziri wake anaeshughulikia masuala ya Brexit, Kwasi Kwarteng akasema ana hakika mwanasheria mkuu Geoffrey Cox ataidhinisha marekebisho hayo:"Nna hakika ataunga mkono mageuzi ya kisheria. Atasema tunaweza kuachana na Backstop tukitaka. Na nna matumaini kutokana na msingi huo DUP, wabunge na wanmachama wa kundi la utafiti kuhusu Ulaya ERG kutoka upande wa wahafidhina nao pia wataunga mkono makubaliano hayo. Sitochoka kusema bunge litabidi lichague leo usiku, ama linaunga mkono makaubaliano ili tusonge mbele au tuendelee  na hali isiyojulikana mwisho na vurugu."

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour, Jeremy CorbynPicha: picture-alliance/AP Photo/UK Parliament/M. Duffy

Labour wanaendelea kupinga

Hata hivyo chama kikuu cha upinzani Labour kimetangaza kitayapinga makubaliano hayo wakihoji "Theresa May" ameshindwa. Kiongozi wa Labour, Jeremy Corbyn anahoji maridhiano yaliyofikiwa hayana chochote cha maana.

Wenye msimamo mkali ndani ya chama cha kihafidhina cha waziri mkuu Theresa May sawa na wanachama wa DUP, chama kidogo cha jimbo la Ireland ya Kaskazini kinachowakilishwa katika serikali ya muungano mjini London wanasema watadurusu kwa makini marekebisho yaliyofikiwa. Kura imepangwa kupigwa usiku. Akishindwa kwa mara nyengine tena, duru ziada za uchaguzi zitahitajika bungeni wiki hii na penegine kusababisha kucheleweshwa mpango wa kujitoa  Brexit au hata kuuakhirisha kwa miezi kadhaa.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/dpa/AFP

Mhariri: Sekione Kitojo