Walinzi wa mbuga walipwe vyema wanapowakamata majangili
17 Mei 2019Baadhi ya wakosoaji wa utaratibu huu wanasema hii ni kuhimiza watu kukamatwa bila makosa, utesaji na mauaji. Kwa hatua hiyo wakosoaji wanasema shirika hilo la WWF linataka kuwasaidia walinzi wa mbuga mbalimbali za wanyama barani Afrika, kutekeleza ukatili dhidi ya raia waishio karibu na mbunga hizo. Na hata wananchi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wanabeba lawama hizo kwa kuwa kodi zao zinasaidia ukatili huo.
"Tunafuatiliwa na kutishiwa, amelalamika mwanamke mmoja wa kabila la Baka katika eneo la bonde la mto Kongo. Wanaharakati wa shirika la kutetea haki za binadamu la Survival International limekuwa likikusanya kwa muda wa miaka mingi kauli hizo za mashahidi na kuandika ripoti ya ukosoaji kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu wanaofanyiwa wakaazi wa asili katika maeneo ya hifadhi ama mbuga za taifa za wanyama katika eneo la misitu ya mvua katika Afrika ya kati. Katika miaka iliyopita malalamiko ya wakaazi wa kabila la Baka yameongezeka.
Eneo lao unakutikana msitu wa Messok Dja katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo , ambao kwa sasa uko chini ya uangalizi wa shirika la ulinzi wa wanyama duniani WWF na kubadilishwa kuwa mbuga ya taifa. Eneo hilo limetengwa maalum kwa kuwalinda sokwe na kuwa ni eneo muhimu kwa kuwalinda tembo barani Afrika. Mradi huo unapata fedha kutoka kwa walipa kodi wa Umoja wa Ulaya na Ujerumani.
Lakini wakaazi wa eneo hilo wanauchukia mradi huo: Watu wa kabila la Baka wanahisi kwamba mbuga hiyo ya taifa inasababisha wao kubughudhiwa. Licha ya kwmba wameishi vizazi na vizazi katika msitu huo wa Messok Dja.
"Mimi ni Mbaka, baba yangu ni Mbaka, mama yangu ni Mbaka. Mababu zetu wametuachia msitu huu. Chakula chetu kinatokana na msitu huu. Tukiwa wagonjwa , tunakwenda msituni kutafuta dawa katika msitu huu, na hata watoto wetu siku zijazo watakwenda kutafuta chakula katika msitu huu. Lakini sasa tumezuiwa kuingia katika msitu huu."
Watu wa kabila la Baka wameporwa uwezo wa maisha yao. Kwa mujibu wa Survival International wakaazi wengi zaidi wa asili katika maeneo ya misituni barani Afrika watakuwa wahanga wa mradi kama huu usio na maadili wa ulinzi wa maeneo ya asili. Shirika hilo limetoa hadharani katika miaka iliyopita kila mara picha mpya, vidio na ushahidi wa maelezo ya wakaazi wenyewe, ambapo limeripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu kupitia mradi huo wa kuwalipa walinzi wa mbunga za wanyama katika mataifa ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Cameroon ama Jamhuri ya Afrika ya kati. Malalamiko hayo kuhusu kamata kamata holela ni pamoja pia na utesaji pamoja na mauaji ya kupangilia.
Moja kati ya malalamiko makubwa , ni kwamba walinzi wa mbuga za wanyama wanapata fedha kwa kila mtu atakayekamatwa. Kutokana na malipo hayo walinzi wa mbuga za wanyama wanapat hamasa zaidi ya kukamata watu wengi zaidi ambao hawana hatia. Linda Poppe wa ofisi ya Survival International mjini Berlin alipozungumza na DW alisema.
"Mfumo huu wa kulipa fedha kwa walinzi wa mbuga za wanyama,unachochea walinzi hao kukamata holela watu na kuongeza matumizi ya nguvu katika eneo hilo. Fedha za kuwalipa walinzi hao katika suala la msitu wa Messok-Dja zinatoka Umoja wa Ulaya."
Serikali ya Ujerumani inatoa fedha kwa ajili ya eneo la bonde la mto Kongo na kuwezesha kile kinachoitwa malipo ya kazi kwa walinzi wa mbuga ya wanyama ya Salonga , ambao pia wanapatiwa fedha hizo maalum. Immo Fischer , msemaji wa WWF nchini Ujerumani akijibu swali la DW amesema:
"Fedha za kuwalipa walinzi wa mbuga za wanyama , ni jambo la kawaida na linatumika katika nchi nyingi za Afrika. Walinzi wa mbuga za wanyama wanafanya kazi za hatari sana, na muhimu sana, na kutokana na kazi hizo muhimu matokeo yake ni malipo."
Mtu anapaswa kutambua kuwa , wazo hili limetokana na haja ya kupunguza rushwa. Wakati mlinzi wa mbunga ya wanyama akimkamata jangili na jangili huyo ana pembe mbili kwa mfano za tembo, malipo yake ya mwaka yataongezeka haraka. Kwa malipo haya kwa walinzi wa mbuga za taifa tunataka kuepuka, kuachiliwa huru kwa majangili kwa kuwapa rushwa walinzi.
Mhariri: Grace Patricia Kabogo
LINK: http://www.dw.com/a-48767929