1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokamatwa na pembe 167 za faru wafikishwa mahakamani

Sekione Kitojo
16 Aprili 2019

Raia wawili wa Afrika Kusini waliokamatwa na pembe 167 za faru, shehena kubwa kabisa kuwahi kurikodiwa na inayoaminika ilikuwa ikisafirishwa kwenda barani Asia, walifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

https://p.dw.com/p/3GtgL
Letzte Nördliche Breitmaulnashorn Weibchen
Picha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Clive John Melville na Petrus Steyn, wote kutoka mji wa kusini wa Port Elizabeth, wanakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa pembe za faru.

Msemaji wa kikosi cha polisi kinachochunguza makosa mahsusi, Hangwani Mulaudzi, alisema wawili hao wangelibakia kizuizini hadi tarehe 26 Aprili siku waliyotazamiwa kuwasilisha maombi ya dhamana.

Polisi ilisema shehena hiyo ya pembe za faru yenye thamani ya kiwango kikubwa cha fedha ilikuwa ikisafirishwa kwenda masoko ya kusini mashariki ya bara la Asia zaidi nchini China na Vietnam.

Afrika Kusini, ambayo ni makaazi ya karibu asilimia 80 ya faru wote duniani, imeathirika vibaya na biashara ya pembe na vipusa ambapo mwaka 2018 pekee, faru 769 waliuwawa na majangili.

AFP, Reuters