1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanadiplomasia wakuu wa Saudia na Iran wakutana China

6 Aprili 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Saudi Arabia wamekutana hii leo mjini Beijing, ikiwa ni ishara ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4PllA
China Peking | Hossein Amir-Abdollahian na Mwanamfalme Faisal bin Farhan Al Saud
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia mwanamfalme Faisal bin Farhan Al SaudPicha: Iran's Foreign Ministry/WANA/REUTERS

Mawaziri wa mambo ya nje waIran na Saudi Arabia wamekutana hii leo mjini Beijing, ikiwa ni ishara ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili yanayogombea ushawishi wa kisiasa na kijeshi katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Mkutano kati ya Hossein Amir-Abdollahian wa Iran na Faisal bin Farhan wa Saudia, ni wa kwanza kuwakutanisha katika kipindi cha zaidi ya miaka saba wajumbe wakuu wa nchi hizo mbili. Rais wa Iran Ebrahim Raisi alisema hivi karibuni kuwa amepokea mwaliko kutoka kwa Mfalme Bin Salman wa Saudia.

Katika makubaliano yaliyosimamiwa na China, Iran na Saudia walikubali mwezi uliopita kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia baada ya miaka mingi ya uhasama. Saudi Arabia ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran kufuatia shambulio la wafuasi wa itikadi kali za kiislamu wa Iran kwenye ubalozi wake mjini Tehran mwaka 2016.