1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 2 wa Iraq na wapiganaji 2 wa Peshmerga wauliuwa

Josephat Charo
23 Oktoba 2023

Duru za jeshi la Iraq na Peshmerga zimesema makabiliano yalidumu muda wa takriban masaa mawili kabla kutulia wakati makamanda wa pande zote walipotaka kutuliza hali ya wasiwasi.

https://p.dw.com/p/4Xsqb
Irak | Ein kurdischer Peschmerga-Kämpfer blickt während heftiger Kämpfe in Bashiqa
Wapiganaji wa PeshmergaPicha: Felipe Dana/AP/picture alliance

Wanajeshi wawili wa Iraq na wapiganaji wawili wa vikosi vya kikurdi vya Peshmerga wameuliwa jana Jumapili wakati pande hizo mbili zilipokabiliana kwenye eneo la milima la kaskazini mwa Iraq. Hayo ni kwa mujibu wa duru za usalama za Iraq na Kurdistan.

Waziri Mkuu wa Iraq na amiri jeshi mkuu Mohammed Shia al-Sudani ameamuru kuundwe kamati maalum kuchunguza mapigano hayo. Duru hizo zimesema wapiganaji wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi, Kurdistan Workers Party PKK walikuwa wameondoka kutoka maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti karibu na mji wa Makhmour siku ya Jumamosi na kuyakabidhi kwa jeshi la Iraq.

Lakini wapiganaji wa Pershmerga wa chama cha Kurdistan Democratic, KDP, chama tawala cha eneo lenye utawala wake wa ndani la Kurdistan, wakajaribu kuyachukua tena maeneo hayo jana Jumapili, na hivyo kuzua mapigano.