1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Nigeria walioshiriki katika kikosi cha UN kuweka amani Liberia wagoma

5 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EWy1

LAGOS

Mamia ya wanajeshi wa Nigeria ambao wametumikia kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa mataifa nchini Liberia wamezusha ghasia kupinga hatua usimamizi wa kijeshi ya kukataa kuwalipa marupurupu yao. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gatezi la Guardian nchini humo wanajeshi hao 323 wanawashutumu maafisa wa kijeshi kwa kutowalipa marupurupu yao tangu waliporejea kutoka nchini Liberia mwezi April.Wanajeshi hao wakiimba nyimbo za vita wakiwa wamebeba fimbo na marungu walifunga barabara kubwa na kuzuia magari na watu kupita katika eneo la kusini mashariki ya mji wa Akure.Hatua hiyo imesababisha hali ya taharuki katika makaazi ya raia wa kawaida katika eneo hilo ambao walilazimika kukaa ndani na kufunga biashara zote.Hadi sasa Maafisa wa kijeshi wanaohusika na suala hilo hajapatikana kuzungumzia hilo.