1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Ujerumani kuendelea kuwepo nchini Afghanistan

Zainab Aziz Mhariri: Daniel Gakuba
26 Machi 2021

Wanajeshi wa Ujerumani wataendelea kuwapo nchini Afghanistan kwa miezi 10 mingine baada ya bunge kuupitisha uamuzi huo kwa mara ya mwisho.

https://p.dw.com/p/3rErZ
Deutschland Diskussion über Wehrpflicht
Picha: picture-alliance/dpa/W. Kumm

Hilo ni swali gumu linaloulizwa na wengi nchini Ujerumani, ikiwa pamoja na familia za wanajeshi takriban 60 waliopelekwa nchini Afghanistan ambako waliuawa. Na bila shaka swali hilo litaendelea kuulizwa baada ya bunge la Ujerumani kuupitisha uamuzi wa kuurefusha kwa miezi 10, muda wa wanajeshi hao kuendelea kuwekwa nchini Afghanistan.

Askari hao waliambiwa kwamba kazi yao haitakuwa ya kuingia katika mapigano bali kuingilia kati kwa muda mfupi kwa lengo la kurejesha utulivu kwenye nchi hiyo iliyokuwamo vitani, nchi ambamo Osama bin Laden alikuwa amejificha. Bin Laden ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda na ndiye  aliyepanga mashambulio ya tarehe 11 mwezi Septemba nchini Marekani. Hata hivyo mambo yaligeuka na kuwa tofauti kabisa.

Wanajeshi wa Ujerumani bado wako nchini Afghanistan kama sehemu ya vikosi vinavyoongozwa na mfungamano wa kijeshi wa NATO kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Afghanistan. Askari wa  Ujerumani 1300 wataendelea kufanya kazi hiyo hadi mwezi Januari mwaka ujao.

Mpaka sasa Ujerumani imeshatumia kiasi cha Euro bilioni 16.4 kwa ajili ya gharama za nchini Afghanistan  hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018. Gharama za jeshi hilo pekee zilifikia kiasi cha Euro biloni 12. Mzigo huo wa gharama umebebwa na walipa kodi.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Annegret Kramp-Karrenbauer
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Annegret Kramp-KarrenbauerPicha: DW

Miaka 20 baada ya mashambulio ya tarehe 11 mwezi Septemba, Marekani sasa inataka kuondoka Afghanistan na kumaliza vita ambavyo vimekuwa vya muda mrefu kwa nchi hiyo kuliko vingine vyote. Ndiyo kusema washirika wa Marekani ikiwa pamoja na Ujerumani nao pia watapaswa kuondoka.

Utawala wa Taliban ulitimuliwa mnamo mwaka 2001 na Bin Laden aliuliwa miaka 10 baadae nchini Pakistan. Jamuhuri ya kiislamu imeundwa nchini Afghanistan, Nchi hiyo ina rais anayechaguliwa na pia bunge linalochaguliwa. Wanawake wanaruhusiwa kufanya kazi na wasichana wanakwenda shule.

Mji wa Kabul umekuwa wa kisasa, internet na simu za kisasa zinanguruma hata hivyo mgogoro bado upo na damu inaendelea kumwagika. Raia zaidi ya 32,000 wameshauawa kutokana na mashambilio ya kigaidi, ya ndege na mapigano yanayoendelea. Watu wengine zaidi ya 60,000 wamejeruhiwa katika muda wa miaka 10 iliyopita.Taliban bado wanadhibiti nusu ya nchi.

Luteni jenerali Carl Hubertus amesema serikali ya Afghanistan haina uwezo wa kudhibiti majimbo yote na kwamba wababe wa kivita ndiyo wenye mamlaka nchini Afghanistan. Wanajeshi wengine wa Ujerumani wamesema walifikiri vita vya nchini Afghanistan vitakuwa vya muda mfupi tu. Wamesema walikuwa kizani kabisa juu ya hali ya nchi hiyo. Luteni jenerali Hubertus amesema amejifunza kwamba askari hawawezi kuleta utulivu wa kudumu katika nchi! Linalotakiwa ni suluhisho la kisiasa na kiuchumi.

Chanzo:/ https://p.dw.com/p/3iI4D