1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasheria wataka Mahakama ya Juu kumshitaki Trump

Mohammed Khelef
9 Aprili 2024

Timu ya mwanasheria maalum wa Marekani, Jack Smith, imeitaka Mahakama ya Juu kuyakataa madai ya rais wa zamani, Donald Trump, kwamba ana kinga ya kutoshitakiwa kwenye kesi ya njama ya kugeuza matokeo ya uchaguzi wa 2020.

https://p.dw.com/p/4eYxh
USA New York | Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.Picha: Yuki Iwamura/AP Photo/picture alliance

Taarifa ya waendesha mashitaka hao iliwasilishwa usiku wa kuamkia Jumanne (Aprili 9) kwenye Mahakama ya Washington, ikiwa ni wiki mbili tu kabla ya majaji kuamua endapo rais huyo huyo wa zamani ashitakiwe ama ala kwa kile alichokitenda wakati akiwa kwenye Ikulu ya White House.

Soma zaidi: Trump aendelea kuisaka kinga dhidi ya makosa yanayomkabili

Wanasheria hao waliiandikia mahakama kwamba njama ya Trump kutaka kutumia madaraka yake kubadili matokeo ya uchaguzi na kuhujumu makabidhiano ya madaraka yalikuwa mambo yanayokinzana kabisa na vifungu vya katiba vinavyoilinda demokrasia ya Marekani.

Uamuzi wa mwisho unatarajiwa tarehe 25 mwezi huu wa Aprili na ndio utakaotowa muelekeo wa kesi hiyo dhidi ya Trump, ikiwa ni takribani miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu, ambao bilionea huyo wa chama cha Republican anatazamiwa kuchuwana tena na Joe Biden wa Democrat.