1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW : Askofu Mpya ajiuzulu

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcW

Askofu Mkuu mpya wa Warsaw aliechaguliwa mwezi uliopita amejiuzulu.

Papa Benedikt amekubali kujiuzulu kwa Askofu huyo Stanislaus Wielgus ambaye alikuwa akitazamiwa kutawazwa rasmi leo hii katika Misa ya Jumapili lakini kukiri kwake huko nyuma kwamba aliwafanyia upelelezi mashushu wa enzi ya ukomunisti nchini Poland kumezusha mtafaruku katika Kanisa Katoliki kwa suala hilo kuwa chanzo cha tahayuri kwa Kanisa.

Kanisa Katoliki la Poland lilitimiza dhima muhimu katika kuupinga ukomunisti nchini humo ambao ulikuja kusambaratika hapo mwaka 1989.

Lakini wanahistoria wanaamini kwamba hadi asilimia 10 ya makasisi yumkini wakawa wametowa ushirikiano wao kwa maafisa wa serikali ya kikomunisti.