1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasaliti walo karibu - Dhuluma za ngono

11 Septemba 2012

Dhulma za kimapenzi ni tatizo kubwa kote barani Afrika. Mchezo huu wa redio unasimulia hadithi ya kusikitisha kuhusu vijana watatu ambao ni waathiriwa wa visa vya unyanyasaji wa kimapenzi.

https://p.dw.com/p/163nD
***Diese Bilder dürfen nur im Zusammenhang mit LBE verwendet werden.*** This series shows how victims of sexual abuse cope with the consequences and find help.
Learning by Ear - Sexual violencePicha: LAIF

Kila mara mtu anaponyanyaswa kimapenzi au hata kubakwa, huwa amedhulumiwa. Dhulma ya aina hii mara nyingi hufanyika kwa usiri mkubwa na wanaodhulumiwa huogopa au wanaona aibu kujitokeza hadharani.  

Katika mchezo huu “Usaliti wa Imani”, tunafuatilia hadithi ya Pato, Nuru na Allan ambao wamedhulumiwa kimapenzi kwa namna moja au nyingine. Pato, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 anajaribu kuficha siri kuhusu tabia ya mwalimu anayemtaka kimapenzi. Lakini anaposhindwa kuvumilia anafichua siri hiyo kwa rafiki zake.

Na katika sehemu nyingine ya nchi hiyo, mashambulizi ya waasi ni jambo la kawaida. Tunakutanna na Nuru, msichana mwenye umri wa miaka 30 ambaye anaishi na makovu  baada ya kubakwa na waasi. Aidha kisa hicho kimeathri maisha yake ya ndoa, kwani mumewe anajihisi mdhaifu na mwenye machungu kuweza kustahamili kisa alichotendewa mkewe.

Kwa upande mwingine kijana Alan mwenye wa umri wa miaka 10 anashindwa kuvumilia na kujitokeza hadharani kumueleza mamake kuhusu ukatili unaotekelezwa na babake wa kambo. Maisha ya vijana hawa watatu ni ya kusikitisha.

Lakini  wanafahamu kwamba wanaweza kupata msaada ili kujikwamua kutoka maisha haya. Mwanamke mmoja jasiri kwa jina, Judy, amezindua shirika la kupambana na dhulma za aina hii “Pambana na Unyanyasaji wa Kimapenzi”  na linakubali kuwasaidia waathiriwa kama Pato, Nuru na Allan.

Sikiliza mchezo huu “Usaliti wa Imani ” ufahamu jinsi vijana hawa watatu walivyojinusuru baada ya visa hivi vya dhulma.

Noa Bongo Jenga maisha yako ni vipindi vinavyotayarishwa na Deutsche Welle na vinasikika katika lugha sita ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi