1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washindi wa nishani ya Nobel wakutana

7 Oktoba 2014

Watunukiwa kumi na mmoja wa nishani ya Nobel watajiunga pamoja wiki hii kutoa tahadhari, wakitangaza kwamba binadamu wanaishi kupindukia uwezo wao na kutia kiwingu katika hali yao ya maisha ya baadaye.

https://p.dw.com/p/1DRcv
Nobelpreisverleihung 2013 Nobelpreis für Physik
Mshindi wa nishani ya Nobel ya fizikia mwaka 2013Picha: Reuters

Katika mkutano mjini Hong Kong unaoingiliana na msimu wa kila mwaka wa tuzo za Nobel, washindi hao wa tuzo hiyo yenye hadhi ya juu kabisa duniani watatoa rai ya kuwapo mapinduzi juu ya binadamu wanavyoweza kuishi, kufanya kazi na kusafiri.

Hali sasa ni ya "maafa" Peter Doherty , mshindi mwenza wa nishani ya Nobel ya madawa mwaka 1996 amesema katika karipio la wazi.

Nobelpreis für Medizin 2013
Nishani ya Nobel ya madawaPicha: Jonathan Nackstrand/AFP/Getty Images

Yeye ni mmoja kati ya washindi 11 wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano wa siku nne kuanzia siku ya Jumatano, mkutano wa nne katika mfululizo wa kongamano la Nobel kuhusiana na hali mbaya ya sayari yetu.

Kuanzia kupanda kwa hali ya joto, kupotea kwa misitu na uharibifu wa udongo na maji hadi kuchafuliwa kwa bahari, uchafuzi wa kemikali na magonjwa yanayozushwa na hali ya mazingira, orodha ya hali mbaya ya sayari yetu ni ndefu na inazidi kuongezeka, Doherty amesema.

Tafakuri inahitajika

Mzozo mkubwa kabisa una maana kwamba walaji, wafanya biashara na watunga sheria wanapaswa kutafakari athari katika sayari yetu kuhusiana na kila uamuzi wanaouchukua, ameliambia shirika la habari la AFP kwa barua pepe.

"Tunahitaji kufikiri kuhusu uendelevu --- uwezo wa kupatikana chakula wakati wote, maji, udongo wenye rutuba, na pia uwezo wa kuwa na hali bora ya hewa.

Ikivuka matangazo ya mwaka 2014 ya tuzo za Nobel kutoka Oktoba 6-13, mkusanyiko wa washindi utalenga katika uwezekano kwamba kupanda kwa hali ya joto duniani kunaweza kufikia mara mbili ya viwango vya ukomo wa Umoja wa Mataifa wa nyuzi joto mbili kupindukia kipindi cha mwanzo wa maendeleo ya viwanda.

Kinachosisisitizwa katika wasi wasi wao ni kuhusu tarakimu mpya zinazoonesha kwamba binadamu anaishi bila kiasi kinyume na uwezo wake.

Binadamu atahitaji sayari nyingine kutosheleza mahitaji yake

Kwa mujibu wa tathmini ya hivi karibuni iliotolewa na wanaharakati wa mazingira wa WWF, binadamu atahitaji sayari 1 na nusu za dunia katika kiwango cha matumizi ya hivi sasa. Kwa maneno mengine , tunatumia zaidi ya asilimia 50 ya mali asili kuliko uasili unavyoweza kutupatia.

Nobelpreis Chemie Thomas A Steitz
Mshindi wa nishani ya Nobel ya kemia Thomas SteitzPicha: AP

"Hali hiyo mbaya ni ya kweli kabisa," amesema mtaalamu wa masuala ya fizikia ya anga Brian Schmidt kutoka Australia, mshindi mwenza wa tuzo ya Nobel ya mwaka 2011 ya fizikia kwa kuonesha ongezeko katika kupanuka kwa ulimwengu.

Kitisho kinatokana na "ongezeko la mahitaji yetu makubwa ya rasilmali, ambayo yanahitajika kuhudumia kiasi cha watu bilioni nane ama zaidi, ambao watakuwa katika sayari hii ya dunia ifikapo mwaka 2050,. wote wakihitaji kuwa na maisha kama yanayopatikana katika mataifa ya magharibi," amesema Schmidt.

"Tunaelekea kufanya uharibifu mkubwa zaidi kwa sayari yetu hii ya dunia katika miaka 35 ijayo kuliko ilivyotokea katika miaka 1,000 iliyopita."

Ada Yonath, , Muisraeli mtaalamu wa masuala ya chembe chembe, mshindi mwenza wa nishani ya Nobel ya kemia mwaka 2009, amesema hali ya endelevu haipaswi tu kuonekana kama uhifadhi wa wanyama na mimea.

Binadamu anapaswa pia kuwa mwangalifu zaidi katika matumizi yake ya rasilmali nyingine zinazosaidia maisha kama viumbe vingine anuai, vinavyoua vijasumu.

Ada Yonath Nobelpreis Chemie 2009
Ada Yonath mshindi wa nishani ya Nobel ya kemia mwaka 2009Picha: AP

Magonjwa sugu

Kusambaa kwa bakteria sugu dhidi ya dawa kutokana na matumizi yasiyo sahihi kumekuwa changamoto muhimu "katika kuendeleza hali ya baadaye ya binadamu," amesisitiza.

Washindi kadhaa wameshauri kulenga katika nishati. Tunapaswa kuachana na matumizi ya mafuta yanayochafua mazingira haraka na kutumia vyanzo salama na , muhimu zaidi , teknolojia mpya zinapaswa kusambazwa haraka katika mataifa yanayoinukia kiuchumi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Caro Robi