1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bunge la Marekani kupinga mpango wa Bush

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcL

Wabunge nchini Marekani wameonya wataupinga mpango mpya wa rais George W Bush kuhusu Irak, unaotarajiwa kuongeza idadi ya wanajeshi.

Ingawa wizara ya ulinzi, Pentagon, imetangaza kuwa mpango wa rais Bush utaongeza wanajeshi Irak, bunge ambalo hivi sasa linaongozwa na chama cha Democrats, limesema rais Bush atatakiwa kueleza sababu kwa nini anahitaji fedha zaidi katika vita nchini Irak.

Gazeti la New York Times liliripoti jana kwamba rais Bush anapania kupeleka wanajeshi 20,000 zaidi mjini Baghdad. Kufikia sasa idadi rasmi ya vifo vya wanajeshi wa Marekani nchini Irak imefikia 3,000.