1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bunge la Marekani limeidhinisha gharama mpya za vita

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByN

Bunge la Marekani,limeidhinisha kutoa Dola bilioni 100 kugharimia vita nchini Iraq na Afghanistan.Wademokrat wanaopinga vita,hapo awali walipendekeza kupanga tarehe ya kuvirejesha nyumbani vikosi vya Marekani,lakini pendekezo hilo limetolewa,baada ya Rais George W.Bush kutumia kura ya turufu.Waliopinga mswada huo bungeni ni Msemaji wa Bunge,Nancy Pelosi wa chama cha Demokrat na wagombea urais wa chama hicho Hillary Clinton na Barack Obama.Uchunguzi wa maoni uliofanywa na CBS na New York Times nchini Marekani,unaonyesha,asilimia 76 ya Wamarekani wanadhani kuwa vita vya Iraq vinakwenda vibaya.