1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush asema kunyongwa kwa Saddam ni hatua muhimu kwa Irak

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCea

Kunyongwa kwa Saddam Hussein kumezusha hisia mbalimbali miongoni mwa viongozi duniani. Rais George W Bush wa Marekani amekueleza kuwa hatua kubwa muhimu kwa Irak.

Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Uingereza, Margaret Beckett, amesema Saddam ameadhibiwa kwa uhalifu alioufanya dhidi ya wairaki.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesema serikali yake inapinga hukumu ya kifo lakini inaheshimu hukumu iliyotolewa dhidi ya Saddam.

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi amesema ana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa machafuko nchini Irak kufuatia kunyongwa kwa Saddam Hussein.

Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, aliyeidhinisha wanajeshi 3,000 wa Italia washiriki katika vita dhidi ya Irak vilivyoongozwa na Marekani, amesema kunyongwa kwa Saddam ni hatua ya kurudisha nyuma maendeleo ya Irak kuelekea demokrasia na ni kosa kubwa la kisiasa na kihistoria.

Baadhi ya mataifa ya kiarabu yamekosoa wakati wa kunyongwa Saddam, ikiwa ni siku ya kwanza ya sherehe za Eid al Adha.