1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush na Olmert watafuta njia za kumuunga mkono Abbas

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqL

Siku moja baada ya Washington kurejesha msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Wapalestina,Rais George W.Bush wa Marekani na Waziri Mkuu wa Israel,Ehud Olmert watakutana kutafuta njia za kumuunga mkono Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas. Viongozi hao wawili wanaamini kuwa serikali mpya ya dharura ya Wapalestina,huenda ikatoa nafasi ya kujadili suluhisho kati ya Waisraeli na Wapalestina.