1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Clinton kugombea urais.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZG

Seneta wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameanzisha nia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza rais wa Marekani.

Clinton alitoa taarifa hizo katika tovuti yake na kusema kuwa ataunda kamati ya uchunguzi ili kugombea kiti cha urais.

Katika ujumbe kwa njia ya video , Clinton amewaalika wapiga kura kuanza mjadala pamoja nae kuhusu masuala muhimu.

Tangazo la Clinton limemaliza miezi kadha ya kukisia. Seneta huyo wa jiji la New York sasa amejiunga na makamu wa rais wa zamani John Edwards na Seneta wa jimbo la Illinois Barack Obama katika kinyang’anyiro hicho kuweza kuteuliwa na chama cha democratic kugombea kiti cha urais. Gavana wa jimbo la New Mexico Bill Richardson nae anatarajia kutangaza mipango yake leo Jumapili.