1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Kamati ya senate yakataa mpango wa Bush

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCY9

Nchini Marekani Kamati yenye nguvu kubwa ya baraza la senate la bunge la Marekani juu ya Uhusiano wa Kigeni imekataa mpango wa Rais George W. Bush wa kutuma wanajeshi wa ziada nchini Iraq.

Kamati hiyo yenye kujumuisha wajumbe wa vyama viwili vikuu vya siasa nchini Marekani ilipiga kura 12 dhidi ya 9 kuunga mkono azmio lisiloshurutisha lenye kuulezea mkakati mpya wa Bush kwa Iraq kuwa na madhara kwa maslahi ya taifa na badala yake kutowa wito wa hatua za kurudisha usalama kwa awamu kukabidhiwa kwa serikali ya Iraq.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Bush kuliomba bunge la Marekani na wananchi wa Marekani kuupa mkakati wake huo mpya nafasi ya kufanya kazi.

Katika hotuba yake ya kwanza ya taifa kwa bunge la Marekani linalodhibitiwa na chama cha Demokrat Bush ameonya kwamba kushindwa nchini Iraq kunaweza kuhatarisha eneo zima la Mashariki ya Kati.