1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rais Bush amteua Robert Zoellick kuwa rais mpya wa benki ya dunia

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwa

Afisa wa ngazi ya juu mjini Washington amesema rais George W Bush amemteua Robert Zoellick, mjumbe wa zamani wa biashara wa Marekani, kuwa rais mpya wa benki ya dunia.

Afisa huyo ameongeza kusema rais Bush anapanga kutangaza uteuzi wake hii leo na anataraji bodi ya magavana wa benki ya dunia imkubali kama kiongozi mpya wa benki hiyo.

Kitadamaduni rais wa benki ya dunia amekuwa mmarekani, lakini miito mingi imekuwa ikitolewa kuwarushu watu wengine duniani wawasilishe maombi yao ya kutaka kuchukua nafasi iliyowachwa na rais wa zamani wa benki hiyo, Paul Wolfowitz.

Wolfowitz alilazika kung´atuka kufuatia kashfa ya kumpandisha cheo na kumuongezea mshahara mpenzi wake, Shaha Riza.

Rais mpya wa benki ya dunia, Robert Zoellick, alifanya kazi kwenye wizara ya mambo ya ndani ya Marekani hadi alipoondoka serikalini mnamo mwaka jana na kujiunga na benki ya uwekezaji ya Goldman Sachs.