1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Rice amekiri makosa katika sera ya Irak

2 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnS

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice amekiri kuwa makosa yamefanywa kuhusu siasa ya Irak.Katika mahojiano yake na stesheni ya televisheni ya Al Arabiya,Rice amesema,bila shaka kuna mambo fulani ambayo yangaliweza kufanywa vingine na serikali yake.